Lugha Nyingine
Makosa ya kimsingi ya kile kinachoitwa “uwezo wa uzalishaji wa China kuliko mahitaji ya soko”
Hivi karibuni, baadhi ya nchi zimehusisha changamoto, kama vile kupungua kwa uwezo wa ushindani wa viwanda vya ndani na kudorora kwa viwanda, na China, zikitekeleza vizuizi mbalimbali dhidi ya nchi hiyo kwa kuvumisha kile kinachoitwa "uwezo wa uzalishaji wa China kuliko mahitaji ya soko."
Ili kukabiliana na mwelekeo huo wa kuingiza siasa katika mambo ya uchumi na biashara, Wizara ya Biashara ya China imechapisha waraka uliopewa kichwa cha "Msimamo wa China kuhusu kile kinachoitwa 'Uwezo wa Uzalishaji kuliko Mahitaji ya Soko" -- waraka wenye maneno karibu 12,000 ambayo kwa kina imekanusha simulizi husika potofu kwa kutumia ukweli halisi wa mambo na takwimu kamili, wakati huohuo umefafanua dhana potofu za jumuiya ya kimataifa.
Kwa kutazama jambo hilo kwa mantiki ya kimsingi ya mfumo wa uchumi wa soko, uwiano kati ya ugavi na mahitaji ya uwezo wa uzalishaji kwa kawaida ni mchakato unaobadilikabadilika. Hakuna uwiano usiobadilikabadilika, na kwa maana hiyo uzalishaji kuliko mahitaji ya soko hauwezi kutambuliwa kwa msingi wa mabadiliko ya muda mfupi ya soko pekee.
Hakuna kigezo kinachotumika duniani kote cha kupima kiwango cha kutumia uwezo wa uzalishaji; kwa nchi zenye uchumi ulioendelea, kwa kawaida kiwango kinachofaa huwa kati ya asilimia 75 na 80, wakati kiwango huwa cha chini zaidi kwa nchi zinazoendelea. Mnamo mwaka 2025, kiwango cha China cha matumizi kikamilifu ya uwezo wa uzalishaji kwa kampuni za viwanda zilizo juu ya ukubwa uliobainishwa kilikuwa asilimia 74.4, na kuiweka katika kiwango kinachofaa. Kiwango hicho hasa kipo juu katika utengenezaji wa hali ya juu na uzalishaji wa sekta inayoibuka, huku kushuka kwa viwango hivyo kwa muda katika viwanda vya jadi, kunatokana na mabadiliko ya muda mfupi yanayotokana na mageuzi ya viwanda na maendeleo ya kijani nchini humo.
Waraka huo umefafanua dhana nne potofu za mara kwa mara. Kwanza, kutoa ruzuku kwa viwanda si sawa na kuchochea uzalishaji kuliko mahitaji. Nchi nyingi duniani hukuza viwanda vinavyoibuka kupitia hatua kama vile uungaji mkono kwa R&D (utafiti na maendeleo) na motisha za kodi. Sera zilizotungwa vizuri za viwanda zinaweza kurekebisha kushindwa kwa soko, na kuchochea maendeleo ya teknolojia za kijani, zenye kutoa kaboni chache na za hali ya juu.
Pili, ziada ya biashara si sawa na uzalishaji unaozidi mahitaji. Nchi nyingi za Ulaya na Marekani kwa miaka mingi zinadumisha ziada za mauzo kwa kiasi kikubwa katika sekta ya utengenezaji bidhaa za kiwango cha juu, wakati China haijawahi kwa makududi kulenga ziada ya mapato ya biashara.
Tatu, madai ya “mahitaji ya ndani kutotosha” yanakinzana na uhalisia wa mambo. Ikipimwa kwa usawa wa nguvu ya ununuzi (PPP), China tayari imeshakuwa soko kubwa zaidi la manunuzi ya bidhaa duniani, ikiongoza dunia katika ununuzi wa bidhaa halisi.
Nne, ushindani mkubwa wa soko wenyewe tu kwa kawaida hudhibiti upanuzi wa uwezo usio na utaratibu. China ambayo ina washiriki zaidi ya milioni 200 wa soko, na idadi kubwa ya kampuni zilizowekezwa kwa mtaji wa kigeni zikipata faida thabiti nchini China, mazingira ya nchi hiyo ya soko lenye ushindani wa haki yanaonekana dhahiri.
Kushuka kwa kiasi kikubwa kwa gharama katika tasnia ya nishati mpya duniani kunachochewa na manufaa yanayosambaa ya uvumbuzi wa mnyororo wa viwanda na uzalishaji wa kiwango kikubwa wa China, hali ambayo imewezesha nchi yoyote duniani kufurahia matunda ya maendeleo ya nishati safi nafuu.
China imetoa waraka huo wa kuonesha msimamo, siyo tu kwa ajili ya kushiriki mjadala wa umma, bali kwa kutetea ushirikiano duniani katika minyororo ya viwanda ili kutimiza maendeleo ya pamoja. Kwa miaka mingi, China imekuwa kila mara ikipanua ufunguaji mlango wake, kwa hatua madhubuti imeshusha viwango vya ushuru, na kurahisisha ufikiaji wa soko katika sekta ya huduma. Ikiwa soko la pili kwa ukubwa wa uagizaji bidhaa duniani, na soko kuu la mauzo ya nchi karibu 80, China inatekeleza utozaji ushuru-sifuri kwa nchi nyingi zinazoendelea, imekuwa ikiandaa maonyesho ya uagizaji bidhaa kwa miaka 8 mfululizo, na inaendelea kufungua uwezekano wa soko lake kubwa la ndani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



