Kitabu kipya cha bluu chaonyesha maendeleo ya intaneti ya AI ya China katika mwaka 2025

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 31, 2026

People's Daily Online imetoa kitabu cha bluu, yaani ripoti ya mwaka juu ya maendeleo ya intaneti ya AI ya China Julai 29. Ripoti hiyo inatoa uchambuzi wa kina wa maendeleo ya AI ya China na inachunguza masuluhisho mahiri ya kivitendo kwa changamoto zinazoibuka.

Ripoti hiyo imechapishwa kila mwaka kwa miaka 12 na ilipewa jina jipya la "Kitabu cha Bluu cha Intaneti ya AI" mwaka 2024 ili kuakisi kongezeka kwa kasi kwa AI. Imeshinda tuzo mbalimbali kutoka Akademia ya Sayansi ya Jamii cha China na inachukuliwa zaidi kuwa kipimo muhimu cha kila mwaka cha kufuatilia maendeleo ya intaneti ya China.

Ripoti hiyo inatoa mapitio ya kina ya intaneti ya AI ya China katika mwaka 2025—mwaka ambao tasnia hiyo inauona kuwa hatua ya mabadiliko ya haraka, wakati teknolojia za AI zilipoibuka kuwa injini kuu ya kuchochea mabadiliko makubwa ya viwanda. Inatazama mazingira ya sera, maendeleo ya kiteknolojia, muundo wa soko na programu tumizi wakilishi, na inaangalia mbele mitindo inayoibuka.

Katika uzinduzi huo, Fan Zhengwei, mkuu wa People's Daily Online, alisisitiza kwamba vyombo vikuu vya habari lazima vikumbatie kikamilifu mabadiliko makubwa ya AI badala ya kungoja uwezeshaji wa kiteknolojia bila kufanya jambo lolote, na kutimiza majukumu yao katika zama ya AI ya kidijitali.

"Mpango wa 15 wa Miaka Mitano unapoanza, intaneti ya AI inafungua fursa mpya kwa vyombo vikuu vya habari. Modeli kubwa na mawakala wanabadilika kuwa msingi mpya wa utambuzi, vikisaidia maudhui kutoka serikali kupitia machaguo ya algoriti na kufikia mamia ya mamilioni ya watumiaji kwa usahihi," Fan amesema.

Amebainisha kuwa data kubwa ya chombo hicho cha habari inayowakilisha mashirika ya mamlaka inaibuka kuwa rasilimali muhimu ya kimkakati kwa ufunzaji wenye ubora wa AI. Amesema AI yenyewe imebadilika kutoka kuwa chombo cha uzalishaji tu hadi kuwa injini yenye nguvu ya biashara, ikichochea vyombo vya habari kuwa washiriki hai katika usimamizi wa AI, uwekaji vigezo, na uwezeshaji wa huduma.

Kwenye uzinduzi huo, mfanyakazi AI wa kidijitali No. 001 wa People's Daily Online pia alijitokeza kwa mara ya kwanza.

Kutolewa kwa kitabu hicho kipya cha bluu kumefuatia kwa karibu baada ya Mkutano wa AI Duniani 2026 (WAIC) na Mkutano wa Ngazi ya Juu Kuhusu Usimamizi wa AI Duniani, uliofanyika Shanghai kuanzia Julai 17-20.

Wakati wa mkutano huo, nchi 29 zilisaini makubaliano ya kuanzisha Shirika la Ushirikiano wa AI Duniani. Kwa mujibu wa shirika la habari la China, Xinhua, China ni kiongozi duniani katika maendeleo ya AI. Mwaka 2025, viwanda vyake vikuu vya AI vilikuwa na thamani ya yuan zaidi trilioni 1.2 (dola za Marekani karibu bilioni 176.6), huku idadi ya kampuni za AI nchini kote ikizidi 6,200.

Maafisa wa serikali, watafiti, mashirikisho ya tasnia na watendaji kutoka kampuni zinazoongoza za intaneti-mahiri pia walishiriki katika majadiliano juu ya kuzidisha maendeleo ya intaneti-mahiri na kujenga aina mpya za uchumi wa AI.

Waangalizi wanabainisha kuwa kitabu hicho cha bluu kinawapa wataalamu wa ndani mapitio ya mwaka ya kimfumo huku kikiwapa wasomaji wa kimataifa dirisha la kujua uchumi wa kidijitali wa China na mwelekeo wa sera yake ya AI, ambalo lisiegemea upande na kuwakilisha mashirika yenye mamlaka.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha