Timu ya madaktari ya China yatoa huduma za kliniki ya bila malipo visiwani Zanzibar, Tanzania

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 27, 2026

Madaktrari wa timu ya madaktari ya China wakifanya uchunguzi wa ultrasaundi kwa mtoto mwenyeji ikiwa ni sehemu ya huduma za utambuzi na matibabu bila malipo wakati wa kliniki ya muda ya wazi kwa umma visiwani Zanzibar, Tanzania, Julai 25, 2026. (Kundi la 35 la timu ya madaktari ya China visiwani Zanzibar, Tanzania/kupitia Xinhua)

Madaktrari wa timu ya madaktari ya China wakifanya uchunguzi wa ultrasaundi kwa mtoto mwenyeji ikiwa ni sehemu ya huduma za utambuzi na matibabu bila malipo wakati wa kliniki ya muda ya wazi kwa umma visiwani Zanzibar, Tanzania, Julai 25, 2026. (Kundi la 35 la timu ya madaktari ya China visiwani Zanzibar, Tanzania/kupitia Xinhua)

DAR ES SALAAM - Kundi la 35 la timu ya madaktari ya China visiwani Zanzibar, Tanzania iliendesha kliniki ya muda ya wazi kwa umma bila malipo visiwani Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya mpango wa "Timu 100 za Madaktari katika Vijiji 1,000" wa China, unaolenga kupanua ufikiaji wa huduma za afya katika ngazi ya jumuiya za makazi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka timu hiyo ya madaktari, kliniki hiyo ilifanyika kwenye Hospitali ya Real Care kaskazini mwa Zanzibar, na kuleta huduma mbalimbali za matibabu kwa wakazi wenyeji.

Timu hiyo, ikiambatana na daktari mwingine Mchina, Dai Shilin kutoka Chuo Kikuu cha Nanjing cha Tiba za Jadi za Kichina, pia ilitoa mashauriano na huduma za matibabu kwa kuweka mkazo zaidi katika magonjwa ya ini, ikiwa ni pamoja na homa ya ini, sambamba na maadhimisho yajayo ya Siku ya Homa ya Ini Duniani.

Dawa maalum za jadi za Kichina zinazofaa kwa hali ya hewa ya kitropiki ya visiwani humo pia zilianza kutolewa rasmi kwa matumizi.

Wajumbe hao madaktari pia walitoa elimu ya afya juu ya kuzuia magonjwa, usimamizi wa magonjwa sugu na matumizi sahihi ya dawa, wakati huohuo wakisambaza dawa zinazotumika mara kwa mara bila malipo.

Bao Zengtao, kiongozi wa timu hiyo ya madaktari, alisema kwamba timu hiyo imeshaendesha kliniki 24 kama hizo mwaka huu, na kufanikisha ufikiajiutoaji wa huduma katika kisiwani kote na kuimarisha ushirikiano wa afya kati ya China na Tanzania.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha