Ethiopia yaahidi kuimarisha ushirikiano wa AI duniani kupitia uanachama wake wa WAICO

(CRI Online) Julai 21, 2026

Serikali ya Ethiopia imesema kwamba uanachama wake katika Shirika la Ushirikiano wa AI Duniani (WAICO) unaonesha dhamira yake ya dhati katika kukuza ushirikiano wa kimataifa katika AI na teknolojia nyingine zinazoibuka.

Wizara ya Uvumbuzi na Teknolojia ya Ethiopia ilisema katika taarifa yake siku ya Jumapili kwamba waziri wake Belete Molla hivi karibuni alisaini makubaliano ya kuanzishwa WAICO mjini Shanghai, China, na kuifanya nchi hiyo kuwa moja ya nchi wanachama 29 waanzilishi wa shirika hilo jipya.

Wizara hiyo imesisitiza kwamba ushiriki wa nchi hiyo katika WAICO unaonesha azma inayokua ya nchi hiyo kwenye AI, mabadiliko makubwa ya kidijitali na ushirikiano wa teknolojia kimataifa.

Julai 16, wanachama kutoka nchi 29 walisaini makubaliano ya kuanzisha WAICO. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alikuwa miongoni mwa wawakilishi kutoka nchi mbalimbali na mashirika ya kimataifa waliohudhuria hafla ya kutia saini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha