UN: Msongamano katika maeneo ya wakimbizi wa ndani umeongeza hatari ya Ebola nchini DRC

(CRI Online) Julai 21, 2026

Ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imeonya Jumatatu kwamba msongamano na upatikanaji mdogo wa huduma za msingi katika maeneo ya wakimbizi wa ndani vinaongeza hatari ya kuenea kwa Ebola mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

OCHA imethibitisha kwamba wagonjwa wa Ebola wameripotiwa katika maeneo yasiyopungua 16 yanayohifadhi wakimbizi wa ndani zaidi ya 270,000 katika jimbo la Ituri, kitovu cha mlipuko huo.

Imesema kuwa Shirika hilo pamoja na washirika wake wanaunga mkono jamii za wakimbizi wa ndani kupitia shughuli za kuzuia na kujenga uelewa, kama vile kuweka vituo vya kunawa mikono na kufanya uhamasishaji wa jamii kuhusu hatua za kuzuia Ebola.

Kwa mujibu wa OCHA hadi kufikia Jumamosi, mamlaka za afya za DRC zilikuwa zimeripoti wagonjwa 2,344 waliothibitishwa kuwa na Ebola katika majimbo matano, Ituri ikichukua asilimia karibu 90 ya wagonjwa hao waliothibitishwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha