Lugha Nyingine
China yachangia chakula cha msaada zaidi ya tani 3,000 kwa Sudan Kusini
China imechangia zaidi ya tani 3,000 za ngano na mchele ili kusaidia watu walio katika mazingira magumu walioathiriwa na ukame, mafuriko na migogoro inayojirudia nchini Sudan Kusini.
Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Jumatatu, waziri wa masuala ya kibinadamu na usimamizi wa majanga wa Sudan Kusini Albino Akol Atak amesema kuwa mchango huo umekuja katika wakati muhimu ambapo nchi hiyo inakabiliwa na misukosuko mingi ya kibinadamu.
Naye Katibu Msaidizi wa Wizara ya Masuala ya Kibinadamu na Usimamizi wa Majanga ya Sudan Kusini William Chan Achuil amesema msaada huo wa chakula utaimarisha kwa kiasi kikubwa usalama wa chakula kwa makundi muhimu, ikiwa ni pamoja na watu waliorejea, wakimbizi wa ndani, watu wenye ulemavu na kaya zilizo katika mazingira magumu nchini kote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



