Uwekaji jiwe la msingi kwa miundombinu muhimu waashiria hatua mpya katika ufufuaji wa TAZARA

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 20, 2026

Katibu Mkuu katika Wizara ya Uchukuzi ya Tanzania Godius Kahyarara akitoa hotuba kwenye hafla ya uwekaji jiwe la msingi jijini Dar es Salaam, Tanzania, Julai 17, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Katibu Mkuu katika Wizara ya Uchukuzi ya Tanzania Godius Kahyarara akitoa hotuba kwenye hafla ya uwekaji jiwe la msingi jijini Dar es Salaam, Tanzania, Julai 17, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

DAR ES SALAAM – Ufufuaji wa Reli ya Tanzania-Zambia (TAZARA) umepata msukumo mpya kupitia hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwa ujenzi wa kituo cha mafunzo na kituo cha usimamizi wa uendeshaji jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Hafla hiyo, iliyofanyika Ijumaa ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuadhimisha miaka 50 tangu reli hiyo ya TAZARA ianze kufanya kazi, iliwakutanisha maafisa waandamizi wa serikali, wanadiplomasia na wadau wa mradi kutoka Tan

Katibu Mkuu katika Wizara ya Uchukuzi ya Tanzania Godius Kahyarara alisema mradi huo unaonyesha dhamira kubwa ya serikali hizo tatu katika kuifufua reli hiyo ya kimkakati.

Alisema kituo hicho cha mafunzo kinaashiria hatua muhimu kuelekea kujenga utaalamu wa reli, ambao utabeba jukumu muhimu zaidi katika sekta ya uchukuzi ya Tanzania na maendeleo mapana zaidi ya kiuchumi.

Li Chongyang, mwenyekiti wa Shirika la Uhandisi wa Ujenzi la China, alisema ujenzi wa vituo hivyo viwili unawakilisha maendeleo halisi katika kutekeleza mradi wa ufufuaji wa TAZARA.

Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian alisema TAZARA ni reli ya urafiki, uhuru na ustawi, akisisitiza mchango wake wa kihistoria katika ukombozi wa kikanda na mafungamano ya kiuchumi.

Alisema mradi huo wa ufufuaji umeingia katika kipindi cha utekelezaji wa kina na unatarajiwa kufungua fursa mpya kwa biashara, maendeleo ya viwanda na uboreshaji wa mambo ya kisasa ya kilimo kando ya njia ya reli hiyo.

“China itaendelea kuunga mkono uendelezaji wa ujuzi na muunganisho wa miundombinu, ikiwemo kupitia ujenzi wa kituo hicho cha mafunzo, ambacho kinatarajiwa kukuza nguvu kazi ya wenyeji wenye ujuzi wa hali ya juu kwa ajili ya uendeshaji na matengenezo ya reli,” aliongeza.

Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA Bruno Ching'andu alisema vituo hivyo viwili vinashughulikia mahitaji mawili ya msingi ya mfumo wa kisasa wa reli: rasilimali watu wenye ujuzi na usimamizi bora wa uendeshaji.

"Kituo cha mafunzo kitaimarisha uwezo wa kiufundi, uendeshaji na usimamizi, wakati kituo cha usimamizi wa uendeshaji kitaboresha uratibu, mawasiliano na usalama katika mtandao mzima wa reli," alisema. 

Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian akitoa hotuba kwenye hafla ya uwekaji jiwe la msingi jijini Dar es Salaam, Tanzania, Julai 17, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian akitoa hotuba kwenye hafla ya uwekaji jiwe la msingi jijini Dar es Salaam, Tanzania, Julai 17, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA Bruno Ching'andu akitoa hotuba kwenye hafla ya uwekaji jiwe la msingi jijini Dar es Salaam, Tanzania, Julai 17, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA Bruno Ching'andu akitoa hotuba kwenye hafla ya uwekaji jiwe la msingi jijini Dar es Salaam, Tanzania, Julai 17, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Wageni wakihudhuria hafla ya uwekaji jiwe la msingi kwa mradi wa ufufuaji wa reli ya TAZARA jijini Dar es Salaam, Tanzania, Julai 17, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Wageni wakihudhuria hafla ya uwekaji jiwe la msingi kwa mradi wa ufufuaji wa reli ya TAZARA jijini Dar es Salaam, Tanzania, Julai 17, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha