Lugha Nyingine
Kliniki ya dawa za jadi za kichina yafunguliwa katika hospitali ya Kibungo nchini Rwanda
Kliniki ya dawa za jadi za Kichina (TCM) imezinduliwa kwenye hospitali ya Kibungo mashariki mwa Rwanda, ikiashiria hatua mpya katika ushirikiano wa muda mrefu wa sekta ya afya kati ya Rwanda na China.
Balozi wa China nchini Rwanda Bw. Gao Wenqi akizungumza Jumatano katika hafla ya uzinduzi, alisema kliniki hiyo inafungua ukurasa mpya katika ushirikiano wa pande mbili.
Amesema kliniki hiyo, ambayo ni ya pili kuanzishwa katika hospitali ya Rwanda, kufuatia ile ya Hospitali ya Masaka, itasaidia kukidhi mahitaji ya matibabu ya jadi ya kichina yanayozidi kuongezeka siku hadi siku katika Hospitali ya Kibungo
Ameongeza kuwa China iko tayari kuimarisha ushirikiano katika sekta ya afya na Rwanda, ili watu wengi zaidi wanufaike na dawa za jadi za Kichina.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



