China yawa mnunuzi wa tatu kwa ukubwa wa kahawa ya Ethiopia

(CRI Online) Julai 17, 2026

Naibu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Kahawa na Chai ya Ethiopia (ECTA) Bw. Shafi Umer, amesema China imekuwa mnunuzi wa tatu kwa ukubwa wa kahawa ya Ethiopia katika mwaka wa fedha wa 2025/26 uliomalizika Julai 7.

Bw. Umer amesema katika mahojiano ya hivi karibuni na Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba China imeipiku Marekani na kuwa mwagizaji wa tatu kwa ukubwa wa kahawa ya Ethiopia, kutoka nafasi ya tano mwaka wa fedha uliopita. Amesema Saudi Arabia na Ujerumani ni nchi ya kwanza na ya pili mtawalia, katika kipindi hicho.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka ECTA, Ethiopia ilisafirisha tani 47,836 za kahawa kwenda kuuza nchini China na kupata dola milioni 347 za Marekani, kutoka tani 34,284 za kahawa na mapato ya dola milioni 219 wakati wa mwaka wa fedha uliopita wa Ethiopia.

“China inaendelea kuwa miongoni mwa masoko mapya ya kahawa ya Ethiopia, lakini tunashuhudia ongezeko la usafirishaji wa kahawa kwenda China, na tuna matumaini kuwa nchi hiyo itakuwa mnunuzi mkubwa zaidi wa kahawa ya Ethiopia katika miaka miwili ijayo,” amesema Umer.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha