China, Tanzania na Zambia zasisitiza ahadi ya kuifufua TAZARA kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya reli hiyo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 16, 2026

Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian akitoa hotuba kwenye hafla ya chakula cha jioni kusherehekea maadhimisho ya miaka 50 tangu Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) ianze shughuli kibiashara jijini Dar es Salaam, Tanzania, Julai 14, 2026. (Xinhua/Nurdin Pallangyo)

Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian akitoa hotuba kwenye hafla ya chakula cha jioni kusherehekea maadhimisho ya miaka 50 tangu Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) ianze shughuli kibiashara jijini Dar es Salaam, Tanzania, Julai 14, 2026. (Xinhua/Nurdin Pallangyo)

DAR ES SALAAM - China, Zambia na Tanzania zimesisitiza ahadi yao ya kuifufua Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kwenye hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika katika jiji la bandari la Dar es Salaam kusherehekea maadhimisho ya miaka 50 tangu Reli hiyo ianze shughuli kibiashara.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Jumanne, Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania Makame Mbarawa ameielezea reli hiyo kuwa ni moja ya mafanikio makubwa zaidi ya maendeleo ya Afrika, yaliyotokana na maono ya hali ya juu, mshikamano usioyumba na urafiki wa kudumu miongoni mwa mataifa.

Alitoa salamu kutoka kwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akisisitiza ahadi ya serikali ya kuimarisha muunganisho wa kikanda na kuhakikisha reli hiyo inabaki kuwa nguzo ya kimkakati kwa ajili ya mabadiliko makubwa ya kiuchumi na ustawi wa pamoja.

Naibu Kamishna Mkuu wa Ubalozi wa Zambia nchini Tanzania Anthony Bwalya amesema kuwa reli hiyo ilibeba jukumu muhimu katika kuhakikisha uhuru wa kiuchumi wa Zambia wakati wa enzi za ukombozi kwa kutoa ufikiaji wa masoko ya kimataifa kupitia bandari ya Bahari ya Hindi ya Dar es Salaam.

Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian amesema kuwa China ilituma wafanyakazi zaidi ya 56,000 wa uhandisi na kiufundi ambao walifanya kazi bega kwa bega na wenzao wa Tanzania na Zambia, akiongeza kuwa bila kuzuiwa na hatari, mambo magumu, au kujitoa mhanga, walijenga reli hiyo pamoja.

Pia amesema kwamba katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, serikali ya China imekuwa ikitoa msaada wa kiufundi na mafunzo kwa wafanyakazi wa usimamizi na kiufundi nchini Zambia na Tanzania. Amesema, kwa hiyo, TAZARA ni ukumbusho wa milele wa urafiki uliojengwa katika kujitoa mhanga na safari ya ushirika ambayo itadumu milele.

Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA Bruno Ching'andu amesema maadhimisho hayo yalihusu vyote viwili kusherehekea na ufufuaji, akisisitiza juhudi zinazoendelea za kuboresha reli hiyo kupitia ushirikiano wa kimkakati na Shirika la Uhandisi wa Ujenzi la China.

Ameeleza kuwa reli hiyo, inayoanzia Dar es Salaam nchini Tanzania hadi New Kapiri Mposhi nchini Zambia, kwa miongo mitano imewezesha biashara, kuunga mkono riziki za watu na kuashiria ushirikiano wa kudumu wa pande tatu kati ya Tanzania, Zambia na China.

Wageni walikuwa wakihudhuria hafla ya chakula cha jioni kusherehekea maadhimisho ya miaka 50 tangu Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kuanza shughuli kibiashara jijini Dar es Salaam, Tanzania, Julai 14, 2026. (Xinhua/Nurdin Pallangyo)

Wageni walikuwa wakihudhuria hafla ya chakula cha jioni kusherehekea maadhimisho ya miaka 50 tangu Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kuanza shughuli kibiashara jijini Dar es Salaam, Tanzania, Julai 14, 2026. (Xinhua/Nurdin Pallangyo)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha