Lugha Nyingine
Trump asema ataondoa mpango wa kutoza ada kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz

Rais wa Marekani Donald Trump (kulia) akimkaribisha Waziri Mkuu wa Iran Ali al-Zaidi kwenye Ikulu ya Marekani, the White House, huko Washington, D.C., Marekani, Julai 14, 2026. (Picha na Li Yuanqing/Xinhua)
WASHINGTON - Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba Marekani itafikia makubaliano ya uwekezaji na nchi za Ghuba badala ya kutoza ada za meli zinazopita kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz.
Trump amesema jana Jumanne katika ujumbe wake kwenye Mtandao wa Truth Social: "Kutokana na mazungumzo yenye ufanisi mkubwa na viongozi wa Mashariki ya Kati, nimeamua kuacha kutoza ada ya asilimia 20 ya kuifidia Marekani na badala yake kufikia makubaliano ya biashara na uwekezaji ambayo nchi mbalimbali za Ghuba zitafanya nchini Marekani."
Trump amesema Mlango-Bahari wa Hormuz utabaki wazi kwa meli zote kupita isipokuwa kwa Iran, wakati huohuo vizuizi vya majini vitaendelea.
"KWA KIASI KIKUBWA, Mlango-Bahari wa Hormuz uko wazi kwa Meli ZOTE kupita isipokuwa kwa Iran," amesema. "Kwa hiyo tutaweka Kizuizi KABISA, lakini kwa Meli zinazoingia na kutoka bandari za Iran tu, au zinazobeba chochote kinachohusiana na mizigo ya Iran," ameongeza.
Uamuzi huo umekuja siku moja baada ya Trump kupendekeza kutoza ada ya asilimia 20 kwa mizigo inayosafirishwa kupitia Hormuz ili kuifidia Marekani kwa kulinda njia hiyo muhimu ya maji.
Trump alisema alikuwa ameliarifu rasmi Baraza la Wawakilishi la Marekani Ijumaa iliyopita kwamba nchi hiyo imeanza tena operesheni za kijeshi dhidi ya Iran.
Mashambulizi mapya ya anga ya Marekani na ulipizaji kisasi wa Iran vimezirudisha Washington na Tehran katika mgogoro wa wazi ndani ya muda usiofikia mwezi mmoja baada ya kusaini makubaliano ya pointi 14 yanayolenga kumaliza vita hivyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



