Kampuni ya China na Chuo cha Confucius vyatoa zana na vifaa vya kielimu kwa shule nchini Ghana

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 13, 2026

Wanafunzi wakishiriki kwenye shughuli ya mawasiliano ya kitamaduni katika Shule ya Kimataifa ya Zenaddo, Accra, Ghana, Julai 10, 2026. (Picha na Seth/Xinhua)

Wanafunzi wakishiriki kwenye shughuli ya mawasiliano ya kitamaduni katika Shule ya Kimataifa ya Zenaddo, Accra, Ghana, Julai 10, 2026. (Picha na Seth/Xinhua)

ACCRA – Kampuni ya Kundi la Uhandisi No.5 la Shirika la Reli la China (CR5) nchini Ghana na Chuo cha Confucius katika Chuo Kikuu cha Ghana (CIUG) vimetoa zana na vifaa vya kielimu kwa shule moja mjini Accra, Ghana ili kuunga mkono mafunzo na masomo ya shule hiyo.

Picha hii iliyopigwa Julai 10, 2026 ikionyesha jengo la Shule ya Kimataifa ya Zenaddo, huko Accra, Ghana. (Picha na Seth/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Julai 10, 2026 ikionyesha jengo la Shule ya Kimataifa ya Zenaddo, huko Accra, Ghana. (Picha na Seth/Xinhua)

Wanafunzi wakitazama klipu ya video ya uhandisi wa barabara wa China kwenye shughuli ya mawasiliano ya kitamaduni katika Shule ya Kimataifa ya Zenaddo, huko Accra, Ghana, Julai 10, 2026. (Picha na Seth/Xinhua)

Wahandisi kutoka Kundi la Uhandisi No.5 la Shirika la Reli la China (CR5) nchini Ghana wakifundisha wanafunzi namna ya kutumia vijiti kujenga daraja kwenye shughuli ya mawasiliano ya kitamaduni katika Shule ya Kimataifa ya Zenaddo, huko Accra, Ghana, Julai 10, 2026. (Picha na Seth/Xinhua)

Vitu vya msaada uliotolewa Ijumaa kwa Shule ya Kimataifa ya Zenaddo vikiwa ni pamoja na televisheni janja, mipira 10 ya miguu, vitabu vya kiada vya lugha ya Kichina, na zana na vifaa vya maabara.

Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya vitu, Liu Baijun, mkurugenzi wa China wa CIUG, alisema kwamba Shule ya Kimataifa ya Zenaddo ni moja ya sehemu za kutoa mafunzo ya lugha ya Kichina ya chuo hicho, na ameongeza kuwa utoaji msaada huo si tu utasaidia kuinua kiwango cha mafunzo ya shule hiyo bali pia utaimarisha urafiki kati ya China na Ghana.

Mwanafunzi akipiga picha kwenye shughuli ya mawasiliano ya kitamaduni katika Shule ya Kimataifa ya Zenaddo, huko Accra, Ghana, Julai 10, 2026. (Picha na Seth/Xinhua)

Mwanafunzi akipiga picha kwenye shughuli ya mawasiliano ya kitamaduni katika Shule ya Kimataifa ya Zenaddo, huko Accra, Ghana, Julai 10, 2026. (Picha na Seth/Xinhua)

Wahandisi kutoka Kundi la Uhandisi No.5 la Shirika la Reli la China (CR5) Tawi la Ghana wakifundisha wanafunzi namna ya kutumia vijiti kujenga daraja kwenye shughuli ya mawasiliano ya kitamaduni katika Shule ya Kimataifa ya Zenaddo, huko Accra, Ghana, Julai 10, 2026. (Picha na Seth/Xinhua)

Shi Shenghai, mhandisi kutoka kampuni hiyo ya China, alisema kwamba Mwaka 2026 wa mawasiliano kati ya Watu wa China na Afrika unatoa fursa kwa kampuni hiyo, kuongeza zaidi ushiriki wake na wakazi katika wakati wa kufanya ujenzi wa miundombinu huko. Kampuni hiyo ya China imeendesha shughuli zake kwa miaka zaidi ya 20 nchini Ghana.

Zenobia Anum-Addo, mkuu wa Shule ya Kimataifa ya Zenaddo, amesema kuwa utoaji msaada huo ni "moyo mwema usiotarajiwa" kutoka kwa mashirika hayo mawili ya China, na shule hiyo ilianzisha masomo ya lugha ya Kichina mwaka mmoja uliopita na wanafunzi wameonyesha shauku kubwa ya kujifunza lugha ya Kichina.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha