Lugha Nyingine
Afrika Kusini yashughulikia wageni zaidi ya 53,000 kwa ajili ya kurejeshwa nyumbani
Afrika Kusini imeshughulikia raia wa kigeni zaidi ya 53,000 kwa ajili ya kuondolewa nchini au kurejeshwa nyumbani kwa kuwezeshwa na serikali, wakati huu ambapo inaongeza juhudi za kusimamia uhamiaji usio rasmi.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari wa Kamati ya Mawaziri juu ya Uhamiaji jana Jumapili mjini Pretoria, Waziri wa Sheria na Katiba wa Afrika Kusini Bw. Mmamoloko Kubayi, amesema hadi kufikia Jumamosi, raia wa kigeni 53,449 walikuwa wamefanyiwa mchakato kwa ajili ya kuondolewa nchini au kurejeshwa nyumbani.
“Wamalawi wanachukua asilimia zaidi ya 80 ya idadi ya jumla, wakifuatiwa na Wazimbabwe na Wamsumbiji.” Amesema Kubayi ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo.
Amesema, idadi ya waliorejeshwa nyumbani kwa nchi zilizo nje ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) ilifikia jumla ya 2,615, ikijumuisha Wanigeria 1,159, Waganda 939, Wakenya 431 na raia 86 wa Jamhuri ya Kongo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



