Lugha Nyingine
China na Namibia zatangaza kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja kwa zama mpya

Rais wa China Xi Jinping na mkewe Peng Liyuan wakipiga picha pamoja na Rais wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah na mumewe Epafras Denga Ndaitwah kabla ya mazungumzo kati ya Xi na Netumbo Nandi-Ndaitwah hapa Beijing, mji mkuu wa China, Julai 10, 2026. (Xinhua/Li Xiang)
BEIJING – Siku ya Ijumaa iliyopita, Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah walipofanya mazungumzo Beijing walitangaza kuwa hadhi ya uhusiano wa pande hizi mbili itainuliwa kuwa jumuiya ya China na Namibia yenye mustakabali wa pamoja kwa zama mpya.
Xi alisema China na Namibia zimekuwa na urafiki mkubwa wa jadi, na matarajio yao kwa maendeleo ni ya pamoja, na aliongeza kuwa tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, kila moja kati ya nchi hizo mbili inachukulia nchi nyingine kuwa ni mshirika wake wenye usawa na zinaungana mkono.
Amedhihirisha kuwa urafiki na ushirikiano wa pande mbili umeendelea kwa kina siku hadi siku, na kuleta manufaa halisi kwa watu wa nchi hizo mbili, Xi alisema China inapenda kubadilishana maoni zaidi na Namibia kuhusu wazo la maendeleo, kufanya uratibu wa mikakati ya maendeleo, na kila upande uwe mshirika wa upande mwingine kwenye njia ya kuelekea mambo ya kisasa.
Xi alitoa mapendekezo matatu ya kujenga jumuiya ya China na Namibia yenye mustakabali wa pamoja kwa zama mpya.
Alisema China na Namibia zinapaswa kudumisha mawasiliano ya karibu kwenye ngazi ya juu, kuzidisha hali ya kubadilishana uzoefu juu ya utawala wa nchi, kuendelea kuwa na mawasiliano kila baada ya muda uliowekwa kuhusu masuala yenye umuhimu wa jumla na wa kimkakati katika uhusiano wa pande mbili, na kuendelea kuungana mkono katika mambo yanayohusiana na maslahi makuu ya kila upande na masuala makubwa yanayofuatiliwa na pande hizo mbili.
Xi pia alitoa mwito wa kuzitaka pande hizo mbili kutumia nguvu zaidi za ushirikiano na kuupelekea kwenye kiwango cha juu zaidi, na ameitia moyo Namibia kutumia vya kutosha ufikiaji wa ushuru-sifuri, njia ya haraka iliyoboreshwa ya mauzo ya nje ya Namibia kwa China, na sera nyingine yenye nafuu.
Xi amesema, "China inapenda kuendeleza kwa kina zaidi ushirikiano wake na Namibia katika ujenzi wa miundombinu, sekta za nishati, madini, kilimo, elimu, vijana, sayansi na teknolojia".
Xi aliongeza kuwa nchi hizo mbili zinapaswa kudumisha mshikamano na uratibu na kulinda kwa pamoja ushirikiano wa pande nyingi. Alisema China inapenda kufanya juhudi za pamoja na nchi za Afrika, ikiwemo Namibia katika kuongeza nguvu na sauti ya Nchi za Dunia ya Kusini, na kutoa mchango mpya kwa ajili ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja. Kwa upande wake, Nandi-Ndaitwah alitoa pongezi za dhati kwa maadhimisho ya miaka 105 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), na akisema, Namibia inatilia maanani sana uhusiano wake na China na inafuata kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja.
"Namibia inakaribisha kampuni zaidi za China kuwekeza na kufanya shughuli zao nchini Namibia, na inatarajia kuimarisha ushirikiano katika sekta za viwanda, madini, miundombinu, usafiri wa anga na anga ya juu, sayansi na teknolojia, kilimo na rasilimali za maji," alisema Nandi-Ndaitwah.
Pande hizo mbili pia zilitoa taarifa ya pamoja kuhusu kujenga jumuiya ya China na Namibia yenye mustakabali wa pamoja kwa zama mpya.
Kabla ya mazungumzo, Xi na mkewe Peng Liyuan walifanya hafla ya kumkaribisha Nandi-Ndaitwah na mumewe Epafras Denga Ndaitwah. Xi na Peng pia walifanya dhifa ya kuwakaribisha jioni.

Rais wa China Xi Jinping akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing kabla ya mazungumzo yao,Julai 10, 2026. (Xinhua/Gao Jie)

Rais wa China Xi Jinping akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, Julai 10, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

Rais wa China Xi Jinping akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, Julai 10, 2026. (Xinhua/Ding Lin)

Rais wa China Xi Jinping akifanya mazungumzo na Rais wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, Julai 10, 2026. (Xinhua/Gao Jie)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



