Mapigano mapya kati ya Marekani na Iran yazua wasiwasi wa kikanda, miito ya kupunguza kupamba moto kwa mvutano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 13, 2026

Picha hii iliyopigwa Juni 20, 2026 ikionyesha Mlango-Bahari wa Hormuz karibu na Khasab, mji mdogo kaskazini mwa Oman. (Xinhua/Wen Xinnian)

Picha hii iliyopigwa Juni 20, 2026 ikionyesha Mlango-Bahari wa Hormuz karibu na Khasab, mji mdogo kaskazini mwa Oman. (Xinhua/Wen Xinnian)

CAIRO - Marekani na Iran zimekabiliana kwa mashambulizi kadhaa mapya juu ya upitaji wa meli kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz jana Jumapili, licha ya nyaraka ya makubaliano iliyosainiwa na nchi hizo mbili mwezi Juni, hali ambayo imeibua wasiwasi juu ya kupamba moto upya kwa mapigano ya kikanda.

Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani imesema katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa X mapema Jumapili kwamba vikosi vyake vilikuwa vimekamilisha mashambulizi ya raundi ya tatu wiki hii (wiki iliyoisha jana Jumapili) dhidi ya Iran, "vikiwawajibisha vikosi vya Iran kwa kushambulia meli nyingine ya kibiashara kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz."

Iran ililipiza kisasi baadaye kwa kulenga kambi na vituo vya Marekani katika nchi mbalimbali za Ghuba, huku vyombo vya habari vya Iran vikisema mashambulizi hayo yalilenga vituo vya kijeshi vya Marekani nchini Kuwait, Bahrain na Qatar.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imesema katika taarifa yake ya jana Jumapili kwamba Misri inalaani mashambulizi hayo ya Iran, ikiyaeleza kuwa ni "ukiukaji mkubwa" wa mamlaka za kitaifa za nchi zilizoathiriwa.

Mashambulizi hayo yanawakilisha "kupamba moto kwa hatari kwa vita ambako kunahatarisha usalama na utulivu wa eneo la Ghuba na kudhoofisha juhudi zinazolenga kupunguza mivutano na kuimarisha usalama wa kikanda," wizara hiyo imesema.

Picha hii iliyopigwa Juni 30, 2026 ikionyesha mandhari ya majengo ya jiji katika eneo la West Bay, Doha, Qatar. (Picha na Nikku/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Juni 30, 2026 ikionyesha mandhari ya majengo ya jiji katika eneo la West Bay, Doha, Qatar. (Picha na Nikku/Xinhua)

Misri imesisitiza kwamba hakuna visingizio au uhalali unaoweza kukubaliwa kwa mashambulizi hayo, ikitoa wito wa kusitishwa mara moja kwa vitendo vyote vinavyofanya hali kupamba moto na kufuata sheria za kimataifa ili kuzuia mvutano na ukosefu wa utulivu zaidi katika eneo hilo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq imeelezea wasiwasi juu ya mivutano na hali ya sasa inayoendelea kuathiri usalama wa baharini katika eneo hilo.

Taarifa ya wizara hiyo imesema kwamba hali hiyo ya sasa inaweza kuwa na athari hasi zinazowezekana kwa usalama na utulivu wa kikanda, vilevile biashara ya kimataifa.

Wajumbe wa Ulinzi wa Raia wa Bahrain wakizima moto uliosababishwa na vifusi vilivyoanguka kutoka kwenye droni za Iran zilizozuiliwa katika Mji wa Hamad, Bahrain, Juni 11, 2026. (Wizara ya Mambo ya Ndani ya Bahrain/kupitia Xinhua)

Wajumbe wa Ulinzi wa Raia wa Bahrain wakizima moto uliosababishwa na vifusi vilivyoanguka kutoka kwenye droni za Iran zilizozuiliwa katika Mji wa Hamad, Bahrain, Juni 11, 2026. (Wizara ya Mambo ya Ndani ya Bahrain/kupitia Xinhua)

Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) pia umelaani mashambulizi hayo ya makombora na droni ya Iran.

Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya UAE imesisitiza mshikamano wa UAE na nchi zinazolengwa na kurudia tena msimamo wa uungaji wake mkono kwa hatua za kulinda usalama na utulivu wao.

Oman jana Jumapili ilimwita balozi wa Iran kutoa taarifa rasmi ya kupinga mashambulizi hayo ya droni yanayolenga maeneo katika majimbo ya Musandam na Al Wusta, Wizara ya Mambo ya Nje ya Oman imesema.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar, katika taarifa yake, imelaani vikali mashambulizi hayo ya Iran yanayolenga eneo lake na nchi kadhaa jirani, ikiyaelezea kuwa ni ukiukaji mkubwa wa mamlaka za kitaifa, ukamilifu wa ardhi na sheria za kimataifa.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha