Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China akutana na Rais wa Namibia mjini Beijing

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Rais wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Julai 9, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)
BEIJING - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amekutana na Rais wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah mjini Beijing jana Alhamisi.
Waziri mkuu Li alisema kuwa Namibia ni mshirika muhimu wa China barani Afrika, China inapenda kushirikiana na Namibia katika kudumisha urafiki wa jadi, kuungana mkono kithabiti maslahi makuu na masuala makubwa yanayofuatiliwa ya kila mmoja, na kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana, ili kusukuma mbele ujenzi wa mambo ya kisasa wa nchi hizo mbili.
Li ametoa wito kwa pande zote mbili kuhusiana na mikakati ya maendeleo katika mwelekeo wa maendeleo na njia za kujiendeleza, na kuungana mkono, vilevile kupanua kiwango cha biashara ya pande mbili, na kuimarisha ushirikiano katika ujenzi wa miundombinu, uchimbaji wa madini, mafuta na gesi, na nishati mpya. kuimarisha ushirikiano katika ujenzi wa miundombinu, uchimbaji wa madini, mafuta na gesi, na nishati mpya.
"China inapenda kuagiza mazao ya kilimo na mazao ya majini yenye sifa bora kutoka Namibia, kuunga mkono kampuni za China zenye uwezo kuwekeza nchini Namibia, na kuitia moyo Namibia kutumia vya kutosha sera ya China ya ushuru-sifuri na sera nyingine ili kupanua mauzo yake ya nje kwa China," Li ameongeza.
Waziri mkuu Li amesema "Pande hizo mbili zinapaswa kuzidisha mawasiliano na ushirikiano katika sekta za utalii, afya, elimu, sayansi na teknolojia, na mawasiliano kati ya vijana," akiongeza kuwa China inapenda kuimarisha uratibu na ushirikiano na Namibia chini ya mfumo wa Umoja wa Mataifa na mifumo mingine na kufanya juhudi pamoja na pande mbalimbali katika kuhimiza ushirikiano wa kweli wa pande nyingi, kutekeleza mapendekezo manne kuhusu dunia yaliyotolewa na China, kusukuma mbele dunia ya ncha nyingi yenye usawa na utaratibu na utandawazi wa uchumi wenye manufaa na ulio jumuishi kwa wote.
Nandi-Ndaitwah, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, amesema upande wa Namibia daima unakumbuka msaada wenye thamani uliotolewa na China kwa Namibia katika mchakato wa kutafuta uhuru na maendeleo ya nchi.
Akidhihirisha kuwa hivi sasa mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano wa pande mbili ni mzuri, akisisitiza Namibia inafuata kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja na inatarajia kufanya juhudi pamoja na China ili kupata matokeo zaidi katika uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote kati ya Namibia na China, na kunufaisha vizuri zaidi watu wa nchi hizo mbili.
"Namibia inatilia maanani sana umuhimu na ushawishi wa China katika mambo ya kimataifa na inapenda kuimarisha mawasiliano na uratibu wa pande nyingi na China, na kuhimiza amani, utulivu na maendeleo ya kikanda," amesema Nandi-Ndaitwah.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Rais wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Julai 9, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



