China yatangaza hatua kukabiliana na hatari za vimbunga na mafuriko

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 08, 2026

Waokoaji wakiwahamisha wakazi waliokwama katika Mji wa Qinzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China, Julai 7, 2026. (Xinhua/Zhang Ailin)

BEIJING - China imetangaza hatua za kudhibiti mafuriko na kukabiliana na dharura wakati huu ambapo vimbunga Maysak na Bavi vikitarajiwa kuleta mvua kubwa na kuongeza zaidi hatari ya mafuriko katika mabonde kadhaa ya mito kote nchini humo, Wizara ya Rasilimali za Maji ya China imesema Jumanne.

Wizara hiyo imefanya mashauriano ili kufanya tathimini ya hali inavyoendelea na athari zinazoweza kusababishwa na vimbunga hivyo viwili na kupanga hatua kwa ajili ya kuzuia mafuriko na kukabiliana na dharura zinazoweza kutokea.

Dhoruba kali za mvua za hivi karibuni zilizosababishwa na Kimbunga Maysak, kimbunga cha 10 kwa mwaka huu, zimesababisha mafuriko makubwa katika maeneo ya Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi kusini mwa China kwenye bonde la Mto Pearl. Kuendelea kwa mvua na mafuriko kunaweza kusababisha hatari zaidi, wizara hiyo imesema.

Mapema Jumanne, mkoa huo wa Guangxi ulipandisha tahadhari yake ya mafuriko hadi tahadhari nyekundu ya kiwango cha juu zaidi, ambayo ilifuatiwa haraka na tahadhari nyingine nyekundu ya mafuriko iliyotolewa na Mkoa jirani wa Guangdong.

Wizara hiyo imesema Kimbunga Maysak kinatarajiwa kuendelea kuiathiri China hadi Julai 9, na kusababisha kuongezeka kwa kiasi kikubwa kwa maji ya mito katika mabonde ya mto Pearl, Changjiang, Huaihe na Songliao, huku mito mingine ikitarajiwa kuzidi viwango vya tahadhari.

Kuanzia Julai 10, Kimbunga Kikubwa Bavi kinatarajiwa kukaribia pwani ya mashariki ya China na kuathiri mabonde sita makubwa ya mito ya nchi hiyo kwa takriban wiki moja, na kuleta hatari kubwa ya maafa yanayotokana na mafuriko.

Wizara hiyo imehimiza juhudi za kuimarisha kuzuia mafuriko katika mkoa huo wa Guangxi, kuboresha mifumo ya ufuatiliaji na tahadhari za mapema, kuhakikisha usalama wa mabwawa ya kuhifadhi maji, kulinda dhidi ya vijito vya milimani na kufurika kwa maji katika mito midogo na ya kati, na kuimarisha ukaguzi wa mitaro na miradi ya kuhifadhi maji.

Waokoaji wakiwahamisha wakazi waliokwama katika Mji wa Qinzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China, Julai 7, 2026. (Xinhua/Zhang Ailin)

Waokoaji wakiwahamisha wakazi waliokwama katika Mji wa Qinzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China, Julai 7, 2026. (Xinhua/Zhang Ailin)

Waokoaji wakiwahamisha wakazi waliokwama katika Mji wa Qinzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China, Julai 7, 2026. (Xinhua/Zhang Ailin)

Waokoaji wakiwahamisha wakazi waliokwama katika Mji wa Qinzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China, Julai 7, 2026. (Xinhua/Zhang Ailin)

Waokoaji wakiwahamisha wakazi waliokwama katika Wilaya ya Binyang ya Nanning, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Kusini mwa China, Julai 7, 2026. (Xinhua)

Waokoaji wakiondoa uzio kuwezesha mashua za uokoaji kupita katika Mji mdogo wa Gantang, Wilaya ya Binyang ya Nanning, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Kusini mwa China, Julai 7, 2026. (Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha