Lugha Nyingine
Watu 11 wafariki, mmoja hajajulikana alipo baada ya dhoruba za radi na upepo mkali kuukumba Mkoa wa Hubei wa China

Wafanyakazi wa usafi wakisafisha njia ya mtaani katika Mji wa Ezhou, Mkoa wa Hubei, katikati mwa China, Julai 6, 2026. (Picha na Zhang Hongbin/Xinhua)
WUHAN – Ofisi husika ya mkoa wa Hubei imesema kuwa, usiku wa jana Jumatatu dhoruba za radi na upepo mkali vilivyotokana na hali mbaya ya hewa kuikumba sehemu ya mashariki mkoani Hubei, katikati mwa China, na kusababisha vifo vya watu 11 na mwingine mmoja hajajulikana alipo.
Ofisi hiyo imesema kati ya saa 1 jioni na saa 5 usiku Jumatatu, dhoruba za radi na upepo mkali viliyakumba maeneo ya Huangshi, Huanggang, Ezhou, na Xianning, ambapo miji midogo miwili ya maeneo hayo ilikumbwa na dhoruba za radi zenye nguvu ya daraja 13. Serikali ya mkoa huo ilisema, hata vimbunga vilitokea katika baadhi ya maeneo.
Ofisi hiyo imeeleza kuwa hali hiyo mbaya ya hewa imesababisha majengo 22 kubomoka, majengo mengine 4,855 kuharibiwa katika eneo hilo, na wakazi wa huko 331wamejeruhiwa.
Hivi sasa mkoa huo umeanza kufanya kazi za uokoaji na utoaji msaada kwa pande zote na kufanya juhudi za kuzuia maafa mengine yanayofuata dhoruba na vimbunga vilivyotokea.

Ofisa wa polisi akiongoza magari katika Mji wa Ezhou, Mkoa wa Hubei, katikati mwa China, Julai 7, 2026. (Picha na Zhang Hongbin/Xinhua)

Ofisa wa polisi akimwelekeza mkazi mmoja kuchukua njia ya mkato katika Mji wa Ezhou, Mkoa wa Hubei, katikati mwa China, Julai 6, 2026. (Picha na Zhang Hongbin/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



