Lugha Nyingine
Mtaalamu wa hali ya hewa wa China Xu Jianmin atunukiwa "Tuzo ya Nobel" ya hali ya hewa

Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Celeste Saulo (kushoto) akitoa Tuzo ya 70 ya Shirika la Hali ya Hewa la Kimataifa (IMO) kwa mtaalamu wa hali ya hewa wa China Xu Jianmin, ambaye pia ni mwanataaluma wa Akademia ya Uhandisi ya China na mtaalamu ongozi wa satalaiti za hali ya hewa anayefanya kazi Mamlaka ya Hali ya Hewa ya China (CMA), mjini Geneva, Uswisi, Juni 24, 2026. (Xinhua/Ma Ruxuan)
GENEVA - Mtaalamu wa hali ya hewa wa China Xu Jianmin, ambaye pia ni mwanataaluma wa Akademia ya Uhandisi ya China na mtaalamu ongozi wa satalaiti za hali ya hewa anayefanya kazi Mamlaka ya Hali ya Hewa ya China (CMA) amekabidhiwa Tuzo ya 70 ya Shirika la Hali ya Hewa la Kimataifa (IMO) mjini Geneva, Uswisi Jumatano wiki hii.
Kwenye hafla ya tuzo hiyo, Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Celeste Saulo amemsifu Xu kwa kujitolea kwake kwa maisha marefu katika kusukuma mbele satalaiti za hali ya hewa na kuhakikisha kwamba data za satalaiti ni zenye kuaminika, za kivitendo, na zenye ufanisi katika kuzitumia.
Saulo amebainisha kuwa chini ya uongozi wa Xu, matumizi ya satalaiti za hali ya hewa za FENGYUN (FY) za China yamepanuka kwa kasi tulivu, wakati huhuo mifumo yake ya uendeshaji imeendelea kuboreshwa, ikitoa uungaji mkono imara kwa ufuatiliaji na utabiri wa hali ya hewa, na ufanyaji maamuzi kwa kutegemea Ushahidi wa hali ya hewa duniani.
Pia amesisitiza jukumu muhimu la satalaiti za FY katika kutoa data za uchunguzi kwa Asia Magharibi, Afrika Mashariki, na eneo la Bahari ya Hindi.
Hasa, uwekaji bora wa satalaiti ya FY-2H kwenye obiti umesaidia kujaza pengo la muda mrefu katika uchunguzi wa hali ya hewa juu ya Bahari ya Hindi kwa kutumia vifaa vya kwenye obiti, na kuunga mkono kwa kiasi kikubwa Mpango wa Ufikiaji Data katika Bahari ya Hindi wa WMO.
Saulo amesifu zaidi kujitolea kwa Xu katika kuwanasihi wanasayansi na wataalamu vijana, vilevile mbinu yake makini, ya kivitendo, na isiyo na ubinafsi katika utafiti wa kisayansi.
Tuzo hiyo ya IMO, inayotolewa kwa mwaka, inachukuliwa kuwa ya heshima ya juu zaidi katika jumuiya ya kimataifa ya hali ya hewa na mara nyingi hujulikana kwa jina la "Tuzo ya Nobel ya hali ya hewa." Tuzo hiyo inatambua michango bora katika hali ya hewa, hidrolojia, na sayansi ya jiofizikia na huwasilishwa kwa mpokeaji mmoja tu kila mwaka.
Xu ni mwanasayansi wa nne wa China kupokea heshima hiyo ya kifahari, baada ya Ye Duzheng, Qin Dahe, na Zeng Qingcheng.

Mtaalamu wa hali ya hewa wa China Xu Jianmin (wa pili, kushoto), ambaye pia ni mwanataaluma wa Akademia ya Uhandisi ya China na mtaalamu ongozi wa satalaiti za hali ya hewa anayefanya kazi Mamlaka ya Hali ya Hewa ya China (CMA) akiwa amekabidhiwa Tuzo ya 70 ya Shirika la Hali ya Hewa la Kimataifa (IMO) mjini Geneva, Uswisi, Juni 24, 2026. (Xinhua/Ma Ruxuan)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



