Mkutano wa usalama wa BRICS wasisitiza ushirikiano wa pande nyingi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 24, 2026

Wang Yi, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya CPC akihudhuria Mkutano wa 16 wa Washauri wa Usalama wa Nchi na Wawakilishi Waandamizi wa Usalama wa Nchi wa BRICS, uliofanyika huko New Delhi, India, Juni 23, 2026. (Xinhua/Javed Dar)

NEW DELHI - Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesema New Delhi, India jana Jumanne kwamba Mkutano wa 16 wa Washauri wa Usalama wa Nchi na Wawakilishi Waandamizi wa Usalama wa Nchi wa BRICS umesisitiza ushirikiano wa pande nyingi.

Wang Yi, amesema washiriki wa mkutano huo wamefikia maoni muhimu ya pamoja kuhusu kushikilia ushirikiano wa pande nyingi, kuhimiza utatuzi wa kisiasa kwa matatizo makubwa, na kufanya uratibu kwa kukabiliana na matishio dhidi ya usalama ya kawaida na yasiyo ya kawaida.

“Mkutano huo pia umeeleza uungaji mkono wa pamoja wa washiriki wa mkutano kwa nchi za BRICS na Nchi za Dunia ya Kusini katika kushikilia kujitawala na kujiamulia, kuongeza mshikamano na kusaidiana, kukusanya hekima ya pamoja, na kuchukua vitendo vyenye nguvu zaidi za pamoja,” amesema Wang.

Ameongeza kuwa, mkutano huo pia umeonyesha washiriki wa mkutano kuunga mkono kutumia zaidi mfumo wa mkutano huo, ili kudumisha mawasiliano na uratibu katika masuala muhimu na matatizo makubwa ya kimataifa na ya kikanda, na kuongezaushirikiano mapana zaidi wa BRICS.

“Mwaka ujao, China itakuwa mwenyekiti wa zamu wa BRICS,” amesema Wang.

Ametumai washiriki wote wa mkutano huo watakutana tena nchini China ili kuzidisha ushirikiano wa kisiasa na usalama kati ya nchi wanachama wa BRICS, na kuchangia hekima na nguvu za BRICS kwa amani na usalama wa dunia.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha