Vance asema Mlango-Bahari wa Hormuz umefunguliwa, Iran kuruhusu wakaguzi wa IAEA kurudi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 23, 2026

Picha iliyopigwa ndani ya chumba cha habari ikimwonyesha Makamu Rais wa Marekani JD Vance akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Buergenstock karibu na Lucerne, Uswisi, Juni 22, 2026. (Xinhua/Lian Yi)

BUERGENSTOCK, Uswisi – Jana Jumatatu Makamu Rais wa Marekani JD Vance amesema huko Buergenstock karibu na Lucerne, Uswisi kwamba Mlango-Bahari wa Hormuz uko wazi na meli za mafuta ghafi na gesi asilia zinapita.

"Tulitaka kuanzisha mfumo wa kudumisha hali ya kufunguliwa wazi kwa Mlango-Bahari wa Hormuz. Sasa mlango huo uko wazi," amesema Vance wakati akitoa hotuba baada ya duru ya kwanza ya mazungumzo kati ya Marekani na Iran kukamilika kwenye hoteli ya Buergenstock katikati mwa Uswisi.

Ameongeza kusema kuwa, bei za gesi na bei za mafuta zinashuka, mamilioni na mamilioni ya mapipa ya mafuta ghafi na gesi asilia yanapita kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz ambayo hayakuwa yakipita hapo awali.

Mlango-Bahari wa Hormuz unapitisha asilimia takriban 20 ya mafuta yanayosafirishwa kwenye njia ya bahari duniani. Iran iliimarisha udhibiti wake kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz baada ya Israeli na Marekani kuanzisha mashambulizi yao ya pamoja dhidi ya Iran Februari 28. Na Marekani iliweka kizuizi cha majini kinacholenga meli zinazoenda na kutoka Iran.

Vance pia amesema kwamba Wairani wamekubali kualika wakaguzi wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) kurudi nchini mwao.

Vance amesema, jambo hili ni “mnara mkubwa”, na ni hatua ya kwanza ya kutimiza hali isiyo na nyuklia nchini Iran na kukomesha milele mpango wa Iran wa silaha za nyuklia. 

Chini ya upatanishi wa Qatar na Pakistan, wajumbe wa mazungumzo wa Marekani na Iran walianza mazungumzo yao Jumapili kwenye hoteli ya mlimani ya Buergenstock katikati mwa Uswisi, hayo ni mazungumzo ya kwanza ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili tangu kusainiwa kwa Nyaraka ya Makubaliano ya Islamabad (MoU) wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa makubaliano ya MoU, Marekani na Iran zinatangaza kukomesha mara moja na kwa daima milele operesheni za kijeshi katika mistari yote ya mbele, ikiwa ni pamoja na Lebanon, na zimeahidi kufanya mazungumzo na kufikia makubaliano ya amani ya mwisho katika kipindi cha siku 60. Vance alisema timu ya Marekani inayofanya mazungumzo na Wairan, Waqatar, na Wapakistan imepata maendeleo makubwa Jumapili.

Amesema timu hiyo itaendelea kufanya kazi katika ngazi ya kiufundi huko Buergenstock na mazungumzo ya kiufundi yataendelea katika wiki kadhaa na siku kadhaa zijazo.

"Tumeweka msingi imara sana kwa ajili ya kufanikisha makubaliano ya mwisho," amesema Vance, akiongeza kuwa bado kuna mengi ya kufanya juu ya mazungumzo ya nyuklia na mazungumzo ya uchumi pamoja na kuondoa mabomu kwenye Mlango Bahari wa Hormuz ili kuhakikisha mtiririko wa vyombo vya majini unaendelea kurudi katika hali ya awali. 

Picha iliyopigwa ndani ya chumba cha habari ikimwonyesha Makamu Rais wa Marekani JD Vance akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Buergenstock karibu na Lucerne, Uswisi, Juni 22, 2026. (Xinhua/Lian Yi)

Picha iliyopigwa ndani ya chumba cha habari ikimwonyesha Makamu Rais wa Marekani JD Vance akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Buergenstock karibu na Lucerne, Uswisi, Juni 22, 2026. (Xinhua/Lian Yi)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha