China yatoa wito wa kugawana kwa usawa manufaa ya kidijitali yanayoendeshwa na AI

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 07, 2026

Fu Cong (mbele), mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa, na Chola Milambo (hayupo pichani), mwakilishi wa kudumu wa Zambia katika Umoja wa Mataifa, wakiongoza kwa pamoja mkutano wa Kundi la Marafiki wa Ushirikiano wa Kimataifa kuhusu Ujenzi wa Uwezo wa AI, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Mei 5, 2026. (Xinhua/Xie E)

UMOJA WA MATAIFA - Fu Cong, mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa, alisema Jumanne wiki hii kwenye mkutano wa Kundi la Marafiki wa Ushirikiano wa Kimataifa kuhusu Ujenzi wa Uwezo wa AI uliofanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani kwamba watu kote duniani wanapaswa kunufaika kwa usawa manufaa ya kidijitali yanayoletwa na akili bandia (AI).

Balozi Fu amesema kuwa katika dunia ya leo, AI inaendelezwa kwa kasi ambayo haijapata kutokea hapo awali na inatumika kwa upana zaidi katika sekta za uchumi na jamii, jambo ambalo linabadilisha mfumo mzima wa maisha ya binadamu na kuwa na umuhimu mkubwa kwa utekelezaji wa Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu.

"Katika mazingira haya, usimamizi wa kimataifa wa akili bandia lazima uendane na maendeleo ya nyakati," amesema.

Amesema kwamba katika kipindi cha miaka miwili iliyopita tangu kuanzishwa kwake, Kundi hilo la Marafiki limeitisha mikutano minne ya wazi na kuandaa warsha tatu za kujenga uwezo wa AI nchini China, zikileta pamoja karibu wawakilishi 200 kutoka nchi wanachama, huku juhudi hizo zikiwawezesha washiriki kushuhudia moja kwa moja maendeleo ya kasi ya AI.

Balozi Fu ametoa wito wa kuzingatia mbinu inayoweka watu kwanza na kuendeshwa na uvumbuzi ili kuwezesha maendeleo ya viwanda kupitia matumizi ya AI+, kujikita katika matokeo halisi, na kulitumia kikamilifu Kundi hilo la Marafiki kama jukwaa la ushirikiano wa kivitendo.

Pia amesisitiza umuhimu wa kulinda mfumo wa ushirikiano wa pande nyingi na kuendeleza mashauriano mapana, mchango wa pamoja, na kunufaishana katika maendeleo ya AI.

Amesema China imejitolea kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu na kusukuma mbele kwa bidii Pendekezo la Usimamizi Duniani na Pendekezo la Usimamizi wa AI Duniani.

"Tuko tayari kushirikiana na pande zote ili kugeuza maono hayo kuwa uhalisia, na kuhakikisha kwamba manufaa ya maendeleo ya AI yanagawiwa kwa upana na kwa usawa zaidi kote duniani," Balozi Fu amesema.

Chola Milambo (kushoto, mbele), mwakilishi wa kudumu wa Zambia katika Umoja wa Mataifa, na Fu Cong (hayupo pichani), mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa, wakiongoza kwa pamoja mkutano wa Kundi la Marafiki wa Ushirikiano wa Kimataifa kuhusu Ujenzi wa Uwezo wa AI, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Mei 5, 2026. (Xinhua/Xie E)

Chen Jiachang (katikati, mbele), naibu waziri wa sayansi na teknolojia wa China, akizungumza kwenye mkutano wa Kundi la Marafiki wa Ushirikiano wa Kimataifa kuhusu Ujenzi wa Uwezo wa AI, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Mei 5, 2026. (Xinhua/Xie E)

Luo Hui (katikati, mbele), mjumbe wa Jumuiya ya Sayansi na Teknolojia ya China, akizungumza kwenye mkutano wa Kundi la Marafiki wa Ushirikiano wa Kimataifa kuhusu Ujenzi wa Uwezo wa AI, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Mei 5, 2026. (Xinhua/Xie E)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha