Lugha Nyingine
China yahimiza mapambano yasimamishwe mashariki mwa DRC
Mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Sun Lei amehimiza jumuiya ya kimataifa kuyafanya mapambano yasimamishwe mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Akihutubia mkutano wa wazi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya eneo la Maziwa Makuu, Balozi Sun amesema, jamii ya kimataifa lazima ihimize pande zote zinazopambana kutekeleza azimio husika la Baraza la Usalama, kuhakikisha ahadi za kusimamisha mapambano zinatekelezwa kivitendo, na kuepukana na hatua zinazoweza kuongeza mvutano.
Pia amesisitiza kuwa China iko tayari kuendelea kushirikiana na pande zote pamoja na nchi za eneo hilo, kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana na nchi za eneo hilo, na kusaidia eneo hilo kutimiza amani ya kudumu na maendeleo yenye ustawi.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma