Lugha Nyingine
Netanyahu asema Israel iko tayari kupambana tena na Iran na itaendelea na mashambulizi dhidi ya Hezbollah
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu tarehe 15 ametoa taarifa kwa njia ya video akisema, Israel iko tayari kupambana tena na Iran, na itaendelea na operesheni za kijeshi dhidi ya Kundi la Hezbollah la Lebanon, huku ikifanya mazungumzo na Lebanon.
Netanyahu amebainisha kuwa Marekani inaendelea kuiarifu Israel kuhusu hali ya mawasiliano kati ya Marekani na Iran, na Israel na Marekani zina lengo moja. Israel inataka uranium nzito ya Iran iondolewe, na kuondoa uwezo wake wa kurutubisha uranium. Israel pia inataka mlango wa bahari unaohusiana na “uchukuzi muhimu wa baharini” ufunguliwe tena.
Netanyahu amesema Israel “iko tayari kukabiliana na hali yoyote” kutokana na uwekezano wa kulipuka tena kwa mapambano, na kwamba Israel inafanya mapambano na Kundi la Hezbollah la Lebanon huku ikifanya mazungumzo na nchi hiyo. Mazungumzo hayo yanalenga kuondoa Kundi la Hezbollah, na kutimiza “amani ya kudumu kupitia uwezo halisi”.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma