Lugha Nyingine
Waziri wa mambo ya nje wa China azungumza na mwenzake wa Iran kwa simu
Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amezungumza na mwenzake wa Iran Bw. Seyed Abbas Araghchi kwa simu jana tarehe 15 Aprili.
Bw. Araghchi amejulisha hali inayohusu mazungumzo ya hivi karibuni kati ya Iran na Marekani, na kueleza kuwa Iran inapenda kupata ufumbuzi halisi kupitia njia ya mazungumzo ya amani. Aidha amesema Iran inapongeza juhudi endelevu za China katika kupunguza mvutano, ikitarajia kuwa China itatoa mchango chanya katika kuhimiza kusitishwa kwa vita na kufikia amani.
Kwa upande wake Bw. Wang Yi amesema kuwa China inaendelea kuiunga mkono Iran katika juhudi zake za kulinda mamlaka, usalama na heshima ya taifa. Rais Xi Jinping wa China ametoa mapendekezo manne ya kudumisha na kuhimiza amani na utulivu katika eneo la Mashariki ya Kati, ambayo yametoa suluhisho la China kwa ajili ya kutatua migogoro. Sasa ni kipindi muhimu cha mpito kutoka kwenye vita kwenda kwenye amani. China inaunga mkono kudumisha mwelekeo wa kusitisha vita na kufanya mazungumzo, jambo ambalo lipo kwenye maslahi ya msingi ya watu wa Iran na pia ni matarajio ya pamoja ya nchi za kikanda na jumuiya ya kimataifa. Uhuru, usalama, na haki na maslahi halali ya Iran kama nchi iliyo kando ya Mlango-Bahari wa Hormuz vinapaswa kuheshimiwa na kulindwa, wakati huohuo usalama na uhuru wa kupita katika Mlango-Bahari huo pia unatakiwa kuhakikishwa, na juhudi za kurejesha upitaji wa kawaida katika mlango huo wa bahari ni matakwa ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa. China inapenda kufuata moyo wa mapendekezo manne yaliyotolewa na rais Xi na kutoa mchango wa kiujenzi kwa utulivu na amani ya kudumu katika eneo la Mashariki ya Kati.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma