Nigeria yazindua makao makuu ya mapato yaliyojengwa na kampuni ya China

(CRI Online) April 16, 2026

Rais wa Nigeria Bola Tinubu amezindua makao makuu mapya ya Huduma za Mapato yaliyojengwa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Abuja, hapo jana.

Jengo hilo la ghorofa 16 lililojengwa na Kampuni ya Ujenzi na Uhandisi ya China (CCECC), liko katikati ya mji huo, na rais Tinubu alielezea kama alama ya kuzaliwa upya kwa hali ya kifedha ya nchi hiyo.

Jengo hilo la kisasa lina uwezo wa kubeba wafanyakazi zaidi ya 3,000, pia lina minara mitatu, ikiwemo kituo cha kuchakata takwimu, maktaba, na ukumbi wa mikutano.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha