China iko tayari kufanya kazi zaidi ya kiujenzi kwa ajili ya amani katika eneo la Ghuba: Waziri Mkuu Li

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 14, 2026

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Sheikh Khaled bin Mohamed bin Zayed Al Nahyan, Mwana Mfalme wa Abu Dhabi, Falme za Kiarabu (UAE), kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Aprili 13, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Sheikh Khaled bin Mohamed bin Zayed Al Nahyan, Mwana Mfalme wa Abu Dhabi, Falme za Kiarabu (UAE), kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Aprili 13, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)

BEIJING - Waziri Mkuu wa China Li Qiang jana Jumatatu alipofanya mazungumzo na Sheikh Khaled bin Mohamed bin Zayed Al Nahyan, mwana mfalme wa Abu Dhabi, Falme za Kiarabu (UAE), mjini Beijing amesema kuwa China iko tayari kufanya kazi zaidi ya kiujenzi na kutoa mchango kwa ajili ya kurejesha amani na utulivu katika eneo la Ghuba.

Waziri Mkuu Li amedhihirisha kuwa tangu mgogoro wa Iran uanze, China imekuwa katika mawasiliano ya karibu na pande husika na kufanya juhudi kubwa katika kuhimiza amani na kukomesha vita.

Waziri Mkuu Li anatumai kwamba UAE itaendelea kuchukua hatua zenye ufanisi ili kuhakikisha usalama wa raia, taasisi na miradi ya China nchini humo.

"Katika miaka ya hivi karibuni, chini ya mwongozo wa kimkakati wa viongozi wakuu wawili wa nchi hizo, uhusiano kati ya China na UAE umeendelea kuzidishwa na kuendelezwa, na ushirikiano katika sekta mbalimbali umepata matokeo mazuri, na kuleta manufaa halisi kwa watu wa nchi zote mbili," Waziri Mkuu Li ameongeza.

Amesema kwamba China ina nia ya kuendelea kushirikiana na UAE katika kufuata njia ya kupata maendeleo kwa pamoja, kuongeza mawasiliano na uratibu, kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa, na kuhimiza uhusiano na ushirikiano kati ya China na UAE ufikie ngazi mpya hatua kwa hatua.

Amesema kwamba China inapenda kushirikiana na UAE katika kuimarisha msingi wa ushirikiano wa nishati, kupanua ushirikiano katika maeneo kama vile uhifadhi wa nishati, nishati ya hidrojeni, magari yanayotumia nishati mpya na betri za umeme, na kuhimiza mabadiliko ya miundo ya kijani ya nchi hizo mbili.

Kwa upande wake, Sheikh Khaled amesema kwamba China ni mshirika muhimu wa kimkakati na rafiki anayeaminika wa UAE, na uhusiano wa pande mbili umewekwa kwenye msingi wa kuaminiana, kuheshimiana na maslahi ya pamoja.

Amesema UAE inaweka umuhimu mkubwa na inatoa kipaumbele cha juu kwenye maendeleo ya uhusiano na China katika sera yake ya mambo ya nje, na inapenda kuimarisha zaidi mawasiliano ya ngazi ya juu na China, kupanua mawasiliano na ushirikiano katika sekta za biashara, uwekezaji, nishati, uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, elimu, utamaduni na nyanja nyingine, ili kuhudumia vizuri maendeleo ya nchi hizo mbili na maslahi ya watu wao.

Baada ya mazungumzo yao, Waziri Mkuu Li na Sheikh Khaled walishuhudia hafla ya kusainiwa kwa nyaraka za ushirikiano katika kilimo, sayansi na teknolojia, uwekezaji na tiba ya jadi ya China.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Sheikh Khaled bin Mohamed bin Zayed Al Nahyan, Mwana Mfalme wa Abu Dhabi, Falme za Kiarabu (UAE), kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Aprili 13, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Sheikh Khaled bin Mohamed bin Zayed Al Nahyan, Mwana Mfalme wa Abu Dhabi, Falme za Kiarabu (UAE), kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Aprili 13, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha