Hafla ya makabidhiano kati ya timu za madaktari wa China nchini Tanzania yafanyika

(CRI Online) April 10, 2026

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

Hafla ya makabidhiano kati ya timu ya 27 na 28 ya madaktari wa China nchini Tanzania imefanyika jana jumatano jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, katibu mkuu wa Wizara ya Afya nchini Tanzania Seif Shekalaghe ameishukuru serikali ya China na timu za madaktari wa China, akizisifia kwa nafasi yake muhimu katika matibabu, uungaji mkono wa kiufundi, na mafunzo.

Naye Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian amesema mpaka sasa, timu 35 za madaktari wa China zimehudumu Zanzibar na 28 Tanzania Bara, na kutoa huduma kwa wagonjwa milioni 20 na kusaidia hospitali za huko kuondoa pengo muhimu la kiufundi.

Mkuu wa timu ya 28 ya madaktari wa China, Liu Jia amesema, watajikita katika mahitaji ya huduma za afya, kutumia uzoefu wao, na kufanya kazi ili kuimarisha uwezo wa huduma za afya, na hivyo kuendeleza zaidi uratibu wa afya kati ya China na Tanzania na kunufaisha jamii za huko.

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha