Lugha Nyingine
Wizara ya Biashara ya China yajibu swali linalofuatiliwa zaidi kuhusu Udhibiti wa Uuzaji wa Nje wa Madini Adimu
Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika tarehe 9, msemaji wa Wizara ya Biashara ya China He Yadong alijibu maswali yaliyofuatiliwa zaidi likiwemo swali kuhusu udhibiti wa uuzaji wa nje wa madini adimu.
Mwandishi wa habari alimwuliza kuwa, kuna ripoti iliyosema kwamba mjumbe wa biashara wa Marekani Jamieson Greer alisema Marekani itafanya mazungumzo na upande wa Beijing, je, kutakuwa na majadiliano na mpango juu ya kuendelea kuahirisha udhibiti wa uuzaji wa nje wa madini ndimu?
He alijibu kuwa, kutokana na maoni yaliyofikia kwa kauli moja katika majadiliano kuhusu mambo ya uchumi na biashara kati ya China na Marekani yaliyofanyika Kuala Lumpur, utekelezaji wa hatua husika za udhibiti wa uuzaji wa nje zilizotangazwa na upande wa China tarehe 9, Oktoba, 2025 utaahirishwa hadi tarehe 10, Novemba 2026. Pande mbili za China na Marekani zitadumisha mawasiliano yao kuhusu masuala yanayofuatiliwa nazo kwa kupitia utaratibu wa mashauriano juu ya mambo ya uchumi na biashara.
Akizungumzia kama Marekani ingekuwa na wasiwasi au la kuhusu China kudhibiti tena uuzaji wa madini adimu kwa Marekani, He alisema, upande wa China siku zote unajitahidi kulinda usalama na utulivu wa minyororo ya uzalishaji na utoaji duniani, kuzingatia vya kutosha mahitaji ya kufaa na ufuatiliaji katika matumizi ya kiraia ya madini adimu duniani, yakiwemo mahitaji ya Marekani, na kuhimiza kwa juhudi na kurahisisha biashara zinazofuata kanuni. Maombi yote ya uuzaji wa nje yanayolingana na masharti ya matumizi ya kiraia yatakubaliwa.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma