Lugha Nyingine
Je, maendeleo ya nyanja za teknolojia zinazoibukia ya China yanakuja kwa gharama ya ustawi wa umma?
Kadri nyanja zinazoibukia za China - kama vile akili mnemba (AI), teknolojia za kidijitali, otomesheni na semikondakta - zinavyostawi, simulizi imeibuka kwamba rasilimali za kitaifa zinakusanywa sana katika sekta za teknolojia ya hali ya juu, zikikandamiza uchumi wa watu kujipatia kipato na hata "kusababisha mzunguko wa uchumi wenye mwelekeo wa kushuka." Hoja ya namna hiyo, kama si jaribio la kupotosha na kuleta mkanganyiko kwa makusudi, basi inaonyesha kushindwa kuelewa kwa kina utaratibu wa msingi wa wimbi jipya la mapinduzi ya kiteknolojia na mageuzi ya kiviwanda.
Watu mara nyingi husema kwamba kile ambacho watu wa kawaida hutafuta si kitu kingine zaidi ya usalama na ustawi. Kauli hii inaweka wazi kwamba usalama unaweka msingi na kuwezesha ustawi. Vile vile, kwa nchi isiyo na usalama wa taifa na kujitegemea kiviwanda, ustawi wa watu unaweza kuwa kama maji bila chanzo au mti usio na mizizi. Hebu fikiria kama China ingekuwa inategemea kabisa chipu zinazoagizwa kutoka nje – mvurugiko wowote wa usambazaji kutoka nje ungetishia uendeshaji wa simu janja, vifaa vya kielektroniki vya matumizi ya nyumbani, magari, na hata miundombinu yote ya kidijitali ya jamii.
Kwa hivyo, kuendeleza kwa juhudi zote nyanja za kimkakati zinazoibukia kama vile semikondakta na anga ya juu si tu ni kuhusu kunyakua fursa zinazojitokeza katika mapinduzi mapya ya kiteknolojia, bali pia ni kuhusu kuandaa aina ya "hakikisho la msingi" kwa maisha ya amani ya watu zaidi ya bilioni 1.4.
Lakini je, nyanja hizo zinazoibukia kiuhalisia zinachukua rasilimali kupita kiasi na kukandamiza ustawi wa umma? Kwanza, nyanja hizi si mashimo meusi ambayo hutumia rasilimali tu bila kutoa pato. Badala yake, zina kiunganishi imara cha kiviwanda na matokeo mazuri ya kusambaa. Baadhi ya uchambuzi unaonyesha kwamba kazi moja kwenye nyanja ya semikondakta inaweza kutoa ajira 5.7 za ziada katika uchumi wenye kuhusiana nayo.
Aidha, maendeleo ya sekta ya teknolojia ya China, ndani yake yenyewe, ni mchakato wa ujumuishaji wa kiteknolojia. Mara tu teknolojia zao zinapokuwa tayari kwa matumizi, zinawezesha nyanja zote na kunufaisha umma kwa ujumla kwa gharama za chini sana. Kwa mfano, mifumo ya upimaji, utambuzi na kutibu magonjwa inayosaidiwa na AI imeboresha kwa kiasi kikubwa uwezo wa kupima, kubaini na kutibu magonjwa wa hospitali za huduma ya msingi.
Shinikizo linalohisiwa na baadhi ya watu kwa sasa halitokani na mabadiliko ya kiteknolojia yenyewe, bali ni kutokana na masuala ya kujifunza upya ujuzi na ya usambazaji wa faida wakati wa mpito kutoka kwenye vichocheo vya ukuaji wa zamani hadi vipya. Tunachopaswa kufanya katika hatua inayofuata si kusimamisha uwekezaji katika sekta ya teknolojia, bali ni kujenga taratibu za uenezaji na mifumo ya usambazaji yenye wepesi na usawa zaidi, ili kuruhusu faida za teknolojia kupenya kwa kasi, upana, na kina zaidi.
Tunaona kwamba kuanzia ngazi za serikali kuu hadi za mitaa, mfululizo wa sera zinatekelezwa kwa kiasi kikubwa: katika kukabiliana na mabadiliko ya kiteknolojia, China inahimiza kwa hamasa mipango ya kuongeza uelewa wa kidijitali na ujuzi miongoni mwa watu wote, na kusaidia wafanyakazi wengi zaidi kuziba pengo la kidijitali.
"Nguvu ya taifa" na "ustawi wa watu" muda wote vimekuwa vikiunganishwa pamoja na kuimarishana. Kila uwekezaji ambao China inafanya leo kwenye teknolojia mpya za kisasa unajenga kasi kwa ajili ya uboreshaji mpana wa ustawi wa watu katika siku za baadaye.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



