Mjumbe wa Bunge la Umma la China Liao Sha: Kulinda “Basi la Furaha” kwa Wanavijiji wa Milimani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 04, 2026

Mjumbe wa Bunge la Umma la China (NPC), Liao Sha, ambaye pia ni kiongozi wa timu ya masoko katika Tawi la Kampuni ya Usafiri wa Umma ya Mji wa Guiyang, hubeba katika begi lake mfano wa basi No. 252 la “Njia Maalumu ya Kunufaisha Wakulima”.

Njia hiyo maalumu ya basi inaunganisha eneo la mjini la Guiyang na vitongoji vyake, likiondoka kila siku saa kumi na mbili na dakika kumi alfajiri kwa wakati. Wakulima wa mboga za majani kutoka vijiji vilivyo kando ya njia hiyo hupakia mboga zao freshi za majani walizovuna punde ndani ya basi hilo na kuziwasilisha hadi kwenye maelfu ya familia mjini.

Kabla ya Juni 2024, wakulima wa mboga za majani kutoka wilayamdogo ya Xiaba mjini Guiyang walilazimika kuondoka nyumbani saa tisa usiku na kutembea gizani kwa saa moja au mbili ili kuwahi basi kwa ajili ya kwenda kuuza mboga zao za majani mjini. Kutokana na kuanzishwa kwa “Njia hiyo Maalum ya Kunufaisha Wakulima” No. 252 sasa wakulima hao wanaweza kufika mapema zaidi katika masoko ya mjini na kupata nafasi nzuri za kuuza bidhaa zao.

Njia hiyo maalum, inayobeba uzito wa “shughuli za kujipatia kipato za wanavijiji”, ni moja ya sehemu ambazo Liao Sha hufanya uchunguzi mara kwa mara.

Kupitia uchunguzi na kutembelea kujionea hali halisi na kwa kutatua “changamoto muhimu”, Liao Sha amefanya juhudi kubwa za kuifanya njia hiyo ya basi kutoa huduma bora kwa wakulima wa mboga za majani. Kuanzia kuanzishwa kwa njia hiyo maalumu na kuboresha njia ya basi hadi kuongeza rafu za kuhifadhia mboga za majani, mfululizo wa hatua hizo si tu zimetatua hatari za kiusalama za usafirishaji wa pamoja wa abiria na mizigo, bali pia zimepunguza muda kwa matunda na mboga za majani kuingia mjini kutoka saa nyingi hadi dakika 40, kupunguza gharama za usafirishaji kwa wakulima, na kuhakikisha mboga freshi zaidi za majani zinafika kwenye meza za wanunuzi.

Mengi ya mabadiliko hayo madogo madogo katika njia za mabasi za Guiyang yanahusiana kwa karibu na matokeo ya utafiti wa Liao Sha.

Wakati huu, Liao Sha ameleta mfano huo wa basi kwenye“Mikutano Mikuu Miwili” ya mwaka huu, akielezea si tu upanuaji wa njia za usafiri, bali pia kuonesha hatua halisi za jinsi upatikanaji sawa wa huduma za umma unavyoweza kuchochea ustawi wa vijijini na kuruhusu wanavijiji wa maeneo ya milimani kunufaika na matunda ya maendeleo ya mijini.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha