Lugha Nyingine
Iran yaonya juu ya mpango wa Israel wa kupanua wigo wa vita katika eneo hilo

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, akizungumza kwenye mkutano wa wiki na waandishi wa habari uliofanyika kwenye shule iliyobomolewa na vita mjini Tehran, Iran, Machi 3, 2026. (Xinhua/Shadati)
TEHRAN/JERUSALEM -- Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, ameonya juu ya mpango wa Israel wa kupanua wigo wa vita na Iran katika eneo lote la Asia Magharibi.
Ametoa kauli hiyo kwenye hotuba yake kwa waandishi wa habari katika mkutano wa wiki na waandishi wa habari uliofanyika kwenye shule iliyobomolewa katika vita mjini Tehran, wakati huohuo akisisitiza kwamba kulifanya eneo hilo la Asia Magharibi kutokuwa salama ni mpango wa Israel.
Baghaei amesema bila shaka Israel inatafuta kutumia vibaya hali ya sasa, kupanua wigo wa vita katika eneo hilo na kutekeleza vitendo vya hujuma katika nchi za kikanda ili kugeuza vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran kuwa mgogoro unaojumuisha pande nyingi katika Asia Magharibi.
Ameelezea matumaini kwamba nchi za Kiislamu na za kikanda zitakuwa macho na kuzuia "vitendo hivyo viovu" vya Israel kuzaa matunda, akisisitiza kwamba uwajibikaji wa pamoja unafanya iwe muhimu kuzuia kuenea kwa mgogoro huo na hali ya ukosefu wa utulivu katika eneo hilo.
Akijibu swali kuhusu ripoti zinazokinzana za Marekani kuomba kumaliza vita, amesema, "Kwa sasa, uwezo na umakini wetu vinajikita pekee katika kulinda nchi.”
Pia Jumanne, Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Gideon Sa'ar alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kukata uhusiano wote wa kidiplomasia na Tehran, akirejelea mashambulizi ya makombora ya hivi punde ya Iran dhidi ya nchi jirani na ukandamizaji wake dhidi ya wapinzani wa ndani.
Akizungumza kwenye mkutano na mabalozi wa kigeni wapatao 60 walioko Israel, Sa'ar amesema kwamba Tehran inaleta tishio linaloenea zaidi ya eneo la sasa la mgogoro wa kijeshi, akitolea mfano zaidi wa uchokozi wa Iran ulioripotiwa kuelekea mataifa ya Ghuba kuwa ni ushahidi wa hatari pana zaidi ya kikanda.
Siku ya Jumamosi asubuhi, mashambulizi ya pamoja ya anga ya Marekani na Israel dhidi ya Tehran na miji mingine ya Iran yalimuua Kiongozi Mkuu Ali Khamenei, pamoja na baadhi ya wanafamilia wa kiongozi huyo, makamanda waandamizi wa kijeshi na raia. Iran ililipiza kupitia mawimbi kadhaa ya mashambulizi ya makombora na droni zilizolenga Israeli na kambi za kijeshi za Marekani katika sehemu mbalimbali za eneo la Mashariki ya Kati.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, akizungumza kwenye mkutano wa wiki na waandishi wa habari uliofanyika kwenye shule iliyobomolewa na vita mjini Tehran, Iran, Machi 3, 2026. (Xinhua/Shadati)

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, akitembea kuingia ndani ya chumba kabla ya mkutano wa wiki na waandishi wa habari uliofanyika kwenye shule iliyobomolewa na vita mjini Tehran, Iran, Machi 3, 2026. (Xinhua/Shadati)

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, akizungumza kwenye mkutano wa wiki na waandishi wa habari uliofanyika kwenye shule iliyobomolewa na vita mjini Tehran, Iran, Machi 3, 2026. (Xinhua/Shadati)

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China

Hong Kong Yasherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa Farasi wa China kwa Maonyesho ya Fataki

Ufunguzi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Milan-Cortina mwaka 2026
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma