Lugha Nyingine
China yatoa wito wa kurudi kwenye mazungumzo juu ya suala la nyuklia la Iran
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning amesema China inatoa wito wa kukomeshwa kwa operesheni za kijeshi na kurudi kwenye meza ya mazungumzo juu ya suala la nyuklia la Iran mapema iwezekanavyo.
Kauli hiyo ya Mao ameitoa jana Jumanne kwenye mkutano na waandishi wa habari. Kabla ya hayo, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) Dr. Rafael Mariano Grossi alisema juzi Jumatatu kwamba hakuna ushahidi kuwa Iran imekuwa ikiendesha mpango wa "kimfumo" wa silaha za nyuklia.
Mao amesisitiza kuwa China ina wasiwasi mkubwa kuhusu Marekani kuishambulia Iran wakati wa mchakato wa mazungumzo, ambayo inakiuka sheria za kimataifa na utaratibu wa kawaida unaoongoza uhusiano wa kimataifa, na ambayo imesababisha kupamba moto kwa ghafla kwa mivutano katika eneo la Mashariki ya Kati.

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China

Hong Kong Yasherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa Farasi wa China kwa Maonyesho ya Fataki

Ufunguzi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Milan-Cortina mwaka 2026
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma