Burundi na UN zasaidia mpango wa dola za kimarekani milioni 82 kurejesha wakimbizi zaidi ya 100,000

(CRI Online) Machi 04, 2026

Serikali ya Burundi na mashirika ya Umoja wa Mataifa zimesaini mpango wa kukabiliana na hali wa dola za kimarekani milioni 82 ili kusaidia kurejehsa wakimbizi 104,000 wa Burundi hadi itakapofika Juni 30.

Hafla ya kusaini mpango huo ilifanyika Jumatatu wiki hii katika mji mkuu wa kibiashara wa Burundi, Bujumbura, na kuhudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Maendeleo ya Jamii na Usalama wa Umma wa Burundi Leonidas Ndaruzaniye, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi Violet Kakyomya, na Mwakilishi wa Kamishna wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa nchini Burundi, Brigette Mukanga-Eno.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Ndaruzaniye amesema lengo kuu la mpango huo ni kuiunga mkono serikali ya Burundi katika usimamizi wa operesheni ya wakimbizi wanaorejea kutoka nchi walizoomba hifadhi kwa ujumla na hususan Tanzania.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha