Trump asema mashambulizi dhidi ya Iran yanaweza “kwenda muda mrefu zaidi” kupita wiki nne hadi tano

(CRI Online) Machi 03, 2026

Rais wa Marekani Donald Trump amesema Jumatatu kuwa operesheni ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Iran ina "uwezo wa kuendelea kwa muda mrefu zaidi" kupita wiki nne hadi tano alizokadiria kwenye mahojiano na waandishi wa habari siku iliyotangulia.

"Tuna uwezo wa kwenda muda mrefu zaidi kuliko huo. Tutafanya hivyo." Trump amesema kwenye hafla moja katika Ikulu ya White House, akirejelea kauli yake ya awali kwamba mashambulizi hayo yanaweza kudumu kwa wiki nne hadi tano.

Naye Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran Bw. Ali Larijani amesema kuwa "tofauti na Marekani, Iran iko tayari kwa vita vya muda mrefu".

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha