Lugha Nyingine
Raia 18 wa China wahamishwa kutoka Iran hadi Azerbaijan

Raia wa China wameondoka kutoka Iran wakijiandaa kupanda basi kwenda Baku kwenye kituo cha ukaguzi wa mpakani cha Astara, kusini mwa Azerbaijan, Machi 1, 2026. (Xinhua/Chen Junfeng)
BAKU – Kutokana na hali ya migogoro inayoendelea kati ya Iran na Marekeni pamoja na Israeli, Raia kumi na wanane wa China wameondoka kutoka Iran hadi Azerbaijan jana Jumapili.
Waandishi wa habari wa Shirika la Habari la China, Xinhua waliokuwa katika kituo cha ukaguzi cha Astara, kusini mwa Azerbaijan kwenye mpaka na Iran walishuhudia Wachina hao walioondoka wakivuka mpaka kuingia nchini Azerbaijan majira ya saa 8:30 mchana kwa saa za huko (10:30 GMT).
Majira ya saa 10:30 jioni kwa saa za huko (12:30 GMT), basi lililokuwa limeandaliwa na Ubalozi wa China nchini Azerbaijan liliondoka katika kituo hicho cha ukaguzi likiwa limebeba kundi la kwanza la waliowasili. Ubalozi wa China nchini humo umesema, watu hao walioondoka watahamishiwa hadi mji mkuu wa Azerbaijan, Baku.
Ubalozi wa China nchini Azerbaijan ulitoa tahadhari ya ubalozi Februari 28, ukisema kwamba utatoa msaada wa lazima kwa raia wa China wanaoingia Azerbaijan au wanaopitia nchi hiyo kurudi nyumbani.

Raia wa China walioondoka kutoka Iran wakipiga picha pamoja kwenye kituo cha ukaguzi wa mpakani cha Astara, kusini mwa Azerbaijan, Machi 1, 2026. (Xinhua/Chen Junfeng)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



