Viongozi wa EAC kukutana nchini Tanzania

(CRI Online) Machi 03, 2026

Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) watafanya mkutano wao wa kawaida wa 25 wa viongozi tarehe 7 mwezi huu jijini Arusha, Tanzania.

Taarifa iliyotolewa na Jumuiya hiyo imesema, mkutano huo wenye kaulimbiu “Kuzidisha Mafungamano kwa ajili ya Kuboresha Maisha ya Raia wa EAC,” utakutanisha viongozi wa nchi nane wanachama watakaotathmini maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya kikanda na kujadili mapendekezo ya kimkakati yanayolenga kuinua ukuaji wa uchumi na kuboresha kiwango cha maisha.

Viongozi hao pia wanatarajiwa kuzindua rasmi Mkakati wa 7 wa Maendeleo wa EAC, ambao unaweka kipaumbele katika kuongeza kasi ya mafungamano na mageuzi ya uchumi na jamii ya kikanda katika miaka mitano ijayo.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha