Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China lamalizika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 03, 2026

Wang Huning, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), akiongoza  kikao cha kufungwa cha mkutano wa 15 wa Kamati ya Kudumu ya  Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China na kutoa hotuba kwenye mkutano huo mjini Beijing, China, Machi 2, 2026. (Xinhua/Ding Lin)

Wang Huning, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), akiongoza kikao cha kufungwa cha mkutano wa 15 wa Kamati ya Kudumu ya kamati ya kitaifa ya CPPCC na kutoa hotuba kwenye kikao hicho mjini Beijing, China, Machi 2, 2026. (Xinhua/Ding Lin)

BEIJING - Mkutano wa 15 wa Kamati ya Kudumu ya kamati ya kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), ambalo ni chombo kikuu cha ushauri wa kisiasa cha China, umefungwa jana Jumatatu mjini Beijing.

Wang Huning, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya CPPCC, aliongoza kikao cha kufungwa cha mkutano huo na kutoa hotuba.

Wang amesema katika mwaka uliopita, kamati ya kitaifa ya baraza hilo imetekeleza majukumu yake kwa makini, kubeba wajibu, kufanya juhudi za kutekeleza hatua, na kupata maendeleo mapya katika kazi yake yote.

Ametoa wito wa kuwataka washauri wa kisiasa kufanya juhudi zaidi mwaka 2026 za kukutoa mashauri na mapendekezo kuhusu utekelezaji wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030), kujenga maoni ya pamoja na kukusanya hekima ili kutoa uhakikisho wa kupata mwanzo mzuri wa utekelezaji wa mpango huo.

Wang pia amesisitiza kutoa nguvu zote za kufanya maandalizi ya mkutano wa nne wa mwaka wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China utakaofunguliwa Machi 4 mjini Beijing.

Kikao hicho cha jana kimepitisha mswada wa ajenda na ratiba ya mkutano wa mwaka, ripoti ya kazi ya Kamati ya Kudumu ya kamati ya kitaifa ya CPPCC, na ripoti kuhusu hali ya kushughulikia mapendekezo yaliyotolewa na washauri wa kisiasa tangu mkutano wa tatu wa wajumbe wote wa baraza hilo.

Nyaraka hizo zitawasilishwa na kuthibitishwa kwenye mkutano wa nne wa mwaka wa kamati ya kitaifa ya CPPCC.

Kikao cha jana kimepiga kura kupitisha orodha ya katibu mkuu na manaibu makatibu wakuu wa mkutano wa nne wa mwaka wa kamati ya kitaifa ya CPPCC.

Kikao hicho pia kimepitisha maamuzi kuhusu ustahiki wa wajumbe kadhaa wa kamati ya kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha