Lugha Nyingine
Wang Yi asema kuunga mkono Iran katika kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi
BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema kwamba China inathamini urafiki wa jadi kati ya China na Iran na inaiunga mkono Iran katika kulinda mamlaka ya nchi, usalama, ukamilifu wa ardhi na heshima yake ya taifa.
Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ameyasema hayo jana Jumatatu wakati akifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyed Abbas Araghchi.
Araghchi ametoa majumuisho ya juu ya hali ya hivi punde ya kikanda, akisema kwamba Marekani imeanzisha vita dhidi ya Iran kwa mara ya pili wakati wa mazungumzo kati ya Iran na Marekani.
Akibainisha kuwa hatua mzuri umepigwa katika duru hii ya mazungumzo kati ya pande hizo mbili, amesema hatua hizo za upande wa Marekani zimekiuka sheria zote za kimataifa na zimekanyaga mstari mwekundu wa Iran.
“Iran haina chaguo ila kujilinda kwa nguvu zake zote,” amesema Araghchi.
Amesema kwamba China imeelezea hadharani msimamo wake wa haki na wa usawa na ana matumaini itaendelea kuchukua jukumu chanya katika kuzuia kupamba moto kwa mvutano katika eneo hilo.
Wang amesisitiza msimamo wa China wa kikanuni juu ya hali ya sasa nchini Iran, akielezea kuiunga mkono Iran katika kulinda haki na maslahi yake halali.
Amesema China imezihimiza Marekani na Israeli kusitisha mara moja operesheni za kijeshi, kuepusha kupamba moto zaidi kwa mvutano, na kuzuia mgogoro huo kusambaa katika eneo la Mashariki ya Kati.
“China inaamini kwamba chini ya hali mbaya na ngumu ya sasa, Iran inaweza kudumisha utulivu wa kitaifa na kijamii, kutilia maanani masuala yenye mantiki yanayofuatiliwa na nchi jirani, na kuhakikisha usalama wa raia na taasisi za China nchini Iran,” amesema Wang.
Araghchi amesema Iran itafanya kila juhudi kuhakikisha usalama wa wafanyakazi na taasisi za China.

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China

Hong Kong Yasherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa Farasi wa China kwa Maonyesho ya Fataki

Ufunguzi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Milan-Cortina mwaka 2026
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma