Lugha Nyingine
China yasema mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran yanakiuka sheria za kimataifa
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning amesema kitendo cha Marekani na Israel kuishambulia kijeshi Iran bila ya idhini ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kimekiuka sheria za kimataifa.
Akijibu swali la waandishi wa habari kuhusu hali ya sasa ya Iran jana Jumatatu, msemaji Mao amesema China inaamini kuwa, mamlaka huru, usalama na ukamilifu wa ardhi wa nchi mbalimbali za Ghuba vinapaswa pia kuheshimiwa kikamilifu.
“Tunazihimiza pande zote kusimamisha opresheni za kijeshi na kuzuia kuenea zaidi kwa mgogoro” amesema.
Pia amesema China inaupongeza msimamo wa mkutano maalumu wa mawaziri wa mambo ya nje wa Baraza la Ushirikiano la Eneo la Ghuba (GCC) kuwa mazungumzo na njia ya kidiplomasia ndiyo njia pekee ya kukabiliana na mgogoro huo kwa sasa na kulinda usalama wa kanda hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



