Chansela wa Ujerumani Merz ahimiza ushirikiano wakati wa kutembelea kampuni nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 27, 2026

Chansela wa Ujerumani Friedrich Merz (katikati) akizungumzana na Ola Kaellenius (kushoto), ofisa mtendaji mkuu wa kundi la Mercedes-Benz, na Cao Xudong, ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya teknolojia ya China Momenta, baada ya kujaribu mfumo wa kusaidia dreva kuendesha gari mjini na kwenye barabara za mwendo kasi, ulioundwa kwa pamoja na Mercedes-Benz na Momenta, mjini Beijing, China, Februari 26, 2026. (Xinhua/Ju Huanzong)

HANGZHOU -- Chansela wa Ujerumani Friedrich Merz alipanda gari jipya la Mercedes-Benz aina ya Class-S kwa ajili ya uendeshaji wa majaribio mjini Beijing asubuhi ya Alhamisi, akijionea mfumo wa kuendesha gari unaosaidiwa na teknolojia ya kisasa katika ziara yake ya kiserikali nchini China.

“Hii ni ya kushangaza. Nadhani ni moja kati ya teknolojia za siku za baadaye kwa ajili ya usafiri,” Merz alisema baada ya kujionea kwake, akipongeza ushirikiano wa karibu kati ya watengenezaji wa Ujerumani na teknolojia ya China.

Mercedes-Benz imeimarisha uwepo wa pande zote hapa na mtandao wa ushirikiano unaoenea mnyororo wake mzima wa kiviwanda nchini China, imesema kampuni hiyo kwenye taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Alhamisi. Timu yake ya utafiti na maendeleo (R&D) ya China inafanya kazi muhimu zaidi katika mtandao wake wa R&D duniani, imesema taarifa hiyo.

Ziara hiyo ya kiserikali ya Merz nchini China ilifanyika Februari 25 na 26. Kutembelea kampuni kutoka nchi zote mbili na kuhimiza ushirikiano wa kivitendo yalikuwa mambo muhimu katika ajenda yake ya Alhamisi.

Merz aliwasili Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China mchana wa Alhamisi. Akiwa katika kampuni ya mambo ya roboti ya Unitree, alitazama roboti zenye umbo la binadamu zikifanya kazi mbalimbali na alivutiwa sana na vitendo vyao sahihi.

Chansela wa Ujerumani Friedrich Merz akijaribu kupanda gari la kizazi kipya aina ya Class-S la Mercedes Benz ili kujionea mfumo wa kusaidia dreva kuendesha gari mjini na kwenye barabara za mwendo kasi, ulioundwa kwa pamoja na Mercedes-Benz na kampuni ya China Momenta, mjini Beijing, China, Februari 26, 2026. (Xinhua/Ju Huanzong)

Chansela wa Ujerumani Friedrich Merz, aliyekuwa kwenye ziara yake ya kiserikali nchini China, akifahamishwa kuhusu maendeleo ya kampuni ya nishati ya Siemens nchini China baada ya kuwasili Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Februari 26, 2026. (Xinhua/Weng Xinyang)

Chansela wa Ujerumani Friedrich Merz, aliyekuwa kwenye ziara yake ya kiserikali nchini China, akitazama roboti yenye umbo la binadamu ya Unitree Robotics ikiandika maandishi ya lugha ya Kichina “Fu”, yanayomaanisha “baraka”, mjini Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Februari 26, 2026. (Xinhua/Weng Xinyang)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha