Lugha Nyingine
Walinzi wa Pwani ya China wafukuza meli za Ufilipino zilizoingia kinyume cha sheria kwenye eneo la bahari la Huangyan Dao

Meli ya Walinzi wa Pwani ya China ya Hebao ikiifukuza kisheria meli ya Ufilipino kwenye eneo la bahari la Huangyan Dao cha China, Bahari ya Kusini ya China, Februari 21, 2026. (Xinhua)
HUANGYAN DAO, Bahari ya Kusini ya China - Walinzi wa Pwani ya China (CCG) siku ya Jumamosi walifukuza meli za Ufilipino zilizoingia kinyume cha sheria kwenye eneo la bahari la China karibu na Huangyan Dao katika Bahari ya Kusini ya China.
Meli kadhaa za Ufilipino zilikuwa zimekusanyika na kuingia kinyume cha sheria karibu na Kisiwa cha Huangyan Dao cha China majira ya mchana wa Februari 21. Meli hizo za Ufilipino zilipiga picha meli za China na kufanya vitendo vya hatari kwa kuvuka njia za meli za CCG zilizokuwa kwenye doria. Na meli ya Walinzi wa Pwani ya Ufilipino No. 4409 pia ilionekana ikizunguka zunguka kule mbali.
Baada ya kupuuzwa kwa utoaji onyo la maneno ya mara kwa mara, meli za CCG zilichukua hatua za udhibiti kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni pamoja na kutoa onyo kwa kupuliza maji kwa nguvu na kudhibiti njia za usafiri, na hatimaye kuzifukuza meli hizo Ufilipino.
Shirika la Habari la China, Xinhua limefahamishwa kutoka eneo husika la operesheni ya kikosi cha meli za CCG kwamba CCG ilishikilia kujizuia na kuchukua hatua kwa busara katika mchakato huo mzima, na hatua zote zikifuata sheria za kimataifa.
Walinzi wa pwani ya China wamesema, ingawa eneo la bahari la Kisiwa cha Huangyan limekabiliwa na hali mbaya ya hewa na ajali za mara kwa mara za baharini hivi karibuni, lakini Ufilipino ingali imekusanya meli nyingi kwenye eneo hilo nyeti, ikifanya onesho kwa kisingizio cha “kulinda usafiri" na “kulinda haki”.
CCG imeongeza kuwa, China siku zote inatekeleza wajibu wake wa uokoaji wa baharini, lakini haitaruhusu nchi yoyote kushambulia mamlaka ya nchi ya China kwa kisingizio chochote.

Picha hii iliyopigwa Februari 21, 2026 ikionyesha meli ya Ufilipino ikiingia kinyume cha sheria kwenye eneo la bahari la Kisiwa cha Huangyan cha China katika Bahari ya Kusini ya China, huku watu kadhaa wa meli hiyo wakishukiwa kuzipiga picha meli za walinzi wa pwani wa China. (Xinhua)

Picha hii ikionyesha meli ya Walinzi wa Pwani ya China ya Hebao ikipuliza maji kwa kuonya meli za Ufilipino zilizoingia kinyume cha sheria kwenye eneo la bahari la Kisiwa cha Huangyan cha China, Bahari ya Kusini ya China, Februari 21, 2026. (Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Februari 21, 2026 ikionyesha meli ya Ufilipino ikiingia kinyume cha sheria kwenye eneo la bahari la Kisiwa cha Huangyan Dao cha China katika Bahari ya Kusini ya China, huku mtu mmoja wa meli hiyo akishukiwa kuzipiga picha meli za walinzi wa pwani wa China. (Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



