Lugha Nyingine
Mkutano Mkuu wa Tisa wa WPK wamchagua Kim Jong Un kuwa katibu mkuu

Mkutano wa Tisa wa Chama cha Workers cha Korea (WPK), chama tawala cha Jamhuri ya Watu ya Kidemokrasia ya Korea, umemchagua Kim Jong Un kuwa katibu mkuu wa chama, Februari 23, 2026. (KCNA/kupitia Xinhua)
PYONGYANG – Mkutano Mkuu wa Tisa wa Chama cha Workers cha Korea (WPK), chama tawala cha Jamhuri ya Watu ya Kidemokrasia ya Korea, umemchagua Kim Jong Un kuwa katibu mkuu wa chama, Shirika Kuu la Habari la Korea (KCNA) limeripoti Jumatatu.
"Mkutano Mkuu wa Tisa wa WPK umeamua kumchagua Kim Jong Un kuwa katibu mkuu wa WPK kutokana na nia thabiti na matakwa ya pamoja ya wajumbe wote, mamilioni ya wanachama wa Chama, watu wote na askari na maofisa wa Jeshi la Umma kwa ajili ya maendeleo ya WPK na ustawi wa nchi," KCNA limeripoti, likinukuu uamuzi uliopitishwa na mkutano huo mkuu juzi Jumapili.
Habari zilizotolewa kwenye mkutano na waandishi wa habari zimeelezwa kuwa mkutano wa Jumapili pia umechagua wajumbe na wajumbe wa akiba wa Kamati Kuu ya WPK, huku Kim Jong Un, Pak Thae Song, Jo Yong Won na Ri Il Hwan wakiwa miongoni mwa wajumbe wa kamati kuu ya Chama waliochaguliwa.
Shirika kuu la habari la KCNA limesema katika habari nyingine kwamba mkutano huo mkuu pia umepitisha uamuzi wa kurekebisha Katiba ya Chama cha WPK.

Mkutano wa Tisa wa Chama cha Workers cha Korea (WPK), chama tawala cha Jamhuri ya Watu ya Kidemokrasia ya Korea, umemchagua Kim Jong Un kuwa katibu mkuu wa chama, Februari 23, 2026. (KCNA/kupitia Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



