Wang Yi asema China iko tayari kushirikiana na nchi zote ili kuboresha usimamizi wa haki za binadamu duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 24, 2026

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akitoa hotuba kupitia njia ya video kwenye kikao cha ngazi ya juu cha Mkutano wa 61 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, mjini Beijing, China, Februari 23, 2026. (Xinhua/Yin Bogu)

BEIJING – Kwenye kikao cha ngazi ya juu cha Mkutano wa 61 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi ametoa hotuba kwa njia ya video akisema kuwa, China iko tayari kushirikiana na nchi zote ili kuboresha usimamizi wa haki za binadamu duniani na kuhimiza maendeleo mazuri ya mambo ya haki za binadamu ya kimataifa.

Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema kuwa hali ya kimataifa ni ngumu na yenye utatanishi, na usimamizi wa haki za binadamu duniani na utaratibu wa kimataifa wa baada ya Vita vya Pili vya Dunia vinakabiliwa na majaribu mapya ya zama hizi.

"Pendekezo la Usimamizi wa Dunia lililotolewa na China limepokea uungaji mkono na majibu kutoka kwa nchi na mashirika ya kimataifa zaidi ya 150," ameongeza.

Wang ametoa wito wa kushikilia usawa wa mamlaka ya nchi na kulinda nia ya awali ya usimamizi wa haki za binadamu duniani. Amesema njia pekee inayoweza kupelekea matarajio mapana zaidi ni njia ile ya maendeleo ya haki za binadamu, njia ambayo inapaswa kukita mizizi katika nchi mbalimbali zenye hali halisi tofauti, na pia inalingana na mahitaji ya watu wake.

"Pande zote zinapaswa kufuata utawala wa sheria wa kimataifa na kuimarisha msingi wa usimamizi wa haki za binadamu duniani. Kwa pamoja, nchi zote zinapaswa kushikilia 'kanuni ya dhahabu' ya kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, na kupinga kithabiti maneno na vitendo vya vigezo viwili kwa kisingizio cha haki za binadamu," amesema.

Ametoa wito wa kufanya ushirikiano wa pande nyingi na kukabiliana na changamoto za usimammizi wa haki za binadamu duniani. Amesema nchi zote zinapaswa kukataa aina zote za ukoloni au ubaguzi wa rangi, na kushughulikia kwa kufaa masuala yanayoibuka kutokana na teknolojia ya AI, mabadiliko ya tabianchi na haki za binadamu. 

Picha hii iliyopigwa Februari 23, 2026 ikimuonyesha Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akitoa hotuba kupitia njia ya video kwenye kikao cha ngazi ya juu cha Mkutano wa 61 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswisi. (Xinhua/Lian Yi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha