Lugha Nyingine
Msumbiji yakaribisha sera ya China ya kutotoza ushuru kwa nchi za Afrika
(CRI Online) Februari 19, 2026
Serikali ya Msumbiji imekaribisha uamuzi wa China wa kutotoza ushuru kwa bidhaa zinazozalishwa kutoka nchi 53 za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia na China, ikibainisha kuwa hatua hiyo ni fursa mpya ya kupanua mauzo ya bidhaa za Afrika kwenye soko la China.
Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari baada ya mkutano wa kila wiki wa Baraza la Mawaziri mjini Maputo, msemaji wa serikali ya Msumbiji Bw. Inocencio Impissa amesema Msumbiji imepokea tangazo hilo "kwa furaha kubwa."
Amebainisha kuwa China na Msumbiji zina uhusiano thabiti, na kuwataka wajasiriamali wa Msumbiji kutumia kikamilifu na fursa zinazoletwa na kuondolewa kwa ushuru, hasa kwa kampuni yanazojihusisha na biashara na mauzo ya nje.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



