Lugha Nyingine
Viongozi wa Afrika watoa mwito wa kubadilisha uwezo wa bara la Afrika kuwa miradi yenye faida
Viongozi wa nchi za Afrika Jumatatu walitoa wito wa pamoja wa kugeuza uwezo mkubwa wa kiuchumi na idadi ya watu wa bara hilo kuwa miradi yenye faida ya kiwango kikubwa na kasi, ili kuhimiza kutimiza malengo ya maendeleo, katika mazingira ya kuongezeka kwa hali ya kutokuwa na uhakika duniani.
Wito huu wa dharura ulitolewa kwenye Jukwaa la 9 la Biashara la Afrika 2026, ambalo ni mkutano mkuu wa biashara wa bara la Afrika, ulioanza Jumatatu mjini Addis Ababa, Ethiopia, chini ya kaulimbiu "Kutoa fedha kwa ajili ya maendeleo ya Afrika: Ajira, Uvumbuzi na Mitaji yenye Ubunifu."
Mkutano huo wa siku mbili, unaoandaliwa kila mwaka na Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA) kwa ushirikiano na Umoja wa Afrika (AU) na wadau wengine, ni jukwaa la kipekee kwa mawasiliano ya ngazi ya juu kati ya viongozi wa nchi za Afrika, viongozi wa sekta binafsi, na wawekezaji.
Mkutano wa mwaka huu umezingatia kuimarisha ushirikiano na kutumia fedha mchanganyiko kuhimiza uchumi wa vijana wa Afrika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



