Madagascar yatangaza "hali ya janga la kitaifa" baada ya Kimbunga Gezani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 14, 2026

Watu wakisafiri kwa mtumbwi kwenye maji ya mafuriko baada ya Kimbunga Gezani kupiga Antananarivo, mji mkuu wa Madagascar, Februari 12, 2026. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

Watu wakisafiri kwa mtumbwi kwenye maji ya mafuriko baada ya Kimbunga Gezani kupiga Antananarivo, mji mkuu wa Madagascar, Februari 12, 2026. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

ANTANANARIVO - Serikali ya Madagascar imetangaza "hali ya janga la kitaifa" Jumatano katika kukabiliana na uharibifu mkubwa uliosababishwa na Kimbunga Gezani.

Kimbunga hicho kimeleta uharibifu mkubwa kwa miundombinu, nyumba na sehemu za kujipatia riziki, sambamba na mafuriko makubwa na hasara kubwa za kiuchumi.

Amri hiyo iliyotangazwa na serikali inarejelea upotevu wa maisha ya watu na kukatizwa kwa jamii kuwa ni sababu kuu. Pia imesema kwamba Kimbunga Gezani kimeathiri vibaya maeneo kadhaa ya Madagascar, na kuzidisha hali mbaya kufuatia Kimbunga Fytia na mvua kubwa inayoendelea.

Serikali sasa imeahidi kutekeleza shughuli za kukabiliana na dharura na utoaji wa misaada, huku ikitoa wito wa dharura kwa ajili ya uungaji mkono wa nchini na kimataifa ili kushughulikia mahitaji ya haraka ya watu walioathiriwa.

Nyumba zilizo kwenye maji zikionekana baada ya Kimbunga Gezani kupiga Antananarivo, mji mkuu wa Madagascar, Februari 12, 2026. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

Nyumba zilizo kwenye maji zikionekana baada ya Kimbunga Gezani kupiga Antananarivo, mji mkuu wa Madagascar, Februari 12, 2026. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha