Mkutano wa Usalama wa Munich wafunguliwa na migongano kati ya pande za Atlantiki yafuatiliwa zaidi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 14, 2026

Hafla ya kufunguliwa kwa Mkutano wa 62 wa Usalama wa Munich (MSC) ikifanyika Munich, Ujerumani, Februari 13, 2026. (Xinhua/Li Ying)

Hafla ya kufunguliwa kwa Mkutano wa 62 wa Usalama wa Munich (MSC) ikifanyika Munich, Ujerumani, Februari 13, 2026. (Xinhua/Li Ying)

MUNICH, Ujerumani - Mkutano wa 62 wa Usalama wa Munich (MSC) umefungtuliwa rasmi jana Ijumaa. Watunga sera kutoka kote duniani wamekusanyika kwenye mkutano huo kujadili usalama wa kikanda na wa dunia na utaratibu wa kimataifa.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mwenyekiti wa MSC Wolfgang Ischinger amesema mkutano huo unafanyika katika wakati wa "hali inayozidi kuwa na wasiwasi," ambapo migogoro na misukosuko yanayotoeka kwa wakati mmoja ni zaidi kuliko wakati wowote katika historia ya miaka zaidi ya 60 iliyopita.

"Uhusiano kati ya pande za Atlantiki hasa unajikuta katika hatua ya msukosuko," Ischinger amesema, akiielezea kuwa ni "changamoto ambayo haijawahi kutokea hapo kabla", na kuhoji kama Marekani bado inawachukulia washirika wa Ulaya kuwa ni washirika.

Akirudia maoni ya wasiwasi huo, Chansela wa Ujerumani Friedrich Merz amesema kwamba "mafarakano" yameonekana kati ya Ulaya na Marekani.

Mkutano huo wa siku tatu wa mwaka huu unatarajiwa kuvutia wakuu wa nchi na serikali takriban 60, vilevile mawaziri wa mambo ya nje na ulinzi wapatao 100.

Mwenyekiti wa Mkutano wa Usalama wa Munich (MSC) Wolfgang Ischinger akihutubia hafla ya kufunguliwa kwa Mkutano wa 62 wa MSC mjini Munich, Ujerumani, Februari 13, 2026. (Xinhua/Li Ying)

Mwenyekiti wa Mkutano wa Usalama wa Munich (MSC) Wolfgang Ischinger akihutubia hafla ya kufunguliwa kwa Mkutano wa 62 wa MSC mjini Munich, Ujerumani, Februari 13, 2026. (Xinhua/Li Ying)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha