Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China aandaa kongamano la wataalamu wa kigeni nchini China

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akiongoza kongamano na wajumbe wa wataalamu wa kigeni waliopewa Tuzo ya Urafiki ya Serikali ya China 2025, pamoja na wataalamu wengine wa kigeni wanaofanya kazi nchini China, kabla ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China Februari 13, 2026. Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang pia alihudhuria kongamano hilo. (Xinhua/Huang Jingwen)
BEIJING - Kabla ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, Waziri Mkuu wa China Li Qiang amefanya kongamano katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing na wajumbe wa wataalamu wa kigeni waliopewa Tuzo ya Urafiki ya Serikali ya China 2025, pamoja na wataalamu wengine wa kigeni wanaofanya kazi nchini China.
Waziri Mkuu Li ametoa salamu za dhati za kila la kheri za Mwaka Mpya wa Jadi kwa wataalamu hao wa kigeni, na kuwashukuru kwa ufuatiliaji wao na uungaji mkono wao kwa ujenzi wa mambo ya kisasa wa China katika muda mrefu uliopita. Pia amesikiliza maoni na mapendekezo yao juu ya maendeleo na kazi za serikali za China.
Wataalamu kutoka nchi za Uingereza, Uholanzi, Uganda, Bulgaria, Belarus na Ujerumani walitoa hotuba juu ya mada zinazohusu uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, maendeleo ya kilimo, na mawasiliano ya kitamaduni , kuwaandaa vipaji na watu wenye ujuzi, pamoja na uwekezaji na ushirikiano.
"Wataalamu wa kigeni wamejenga taaluma zao nchini China, na mafanikio ya kivumbuzi na matokeo ya kazi zao yameleta manufaa kwa China, na pia yananufaisha Dunia," Waziri Mkuu Li amesema.
Amesema kwamba mapendekezo ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China kuhusu maandalizi ya Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030), yameweka ramani kubwa ya maendeleo ya China katika miaka mitano ijayo. Amewatia moyo wataalamu hao wa kigeni kutumia fursa hii, kuendelea kushiriki na kufanya juhudi kwa pamoja kwa ajili ya mustakabali bora, na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya maendeleo ya ustaarabu wa binadamu.
"Wataalamu wa kigeni wanaofanya kazi nchini China ni marafiki wa dhati wa watu wa China," Waziri Mkuu Li amesema, akisisitiza kwamba serikali ya China itajitahidi kujenga mazingira mazuri zaidi kwa maisha na kazi zao, na itaendelea kulinda amani na utulivu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



