Lugha Nyingine
Netanyahu aeleza mashaka kuhusu uwezekano wa makubaliano kati ya Marekani na Iran, atoa wito wa kudhibiti makombora
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian akizungumza kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 47 tangu kufanyika Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979 mjini Tehran, Iran, Februari 11, 2026. (Xinhua/Shadati)
CAIRO - Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema jana Alhamisi kwamba "alieleza mashaka ya jumla kuhusu hali ya makubaliano yoyote na Iran" na kama makubaliano kati ya Marekani na Iran yatafikiwa, lazima yanahusisha "makombora ya masafa marefu na makundi ya wakilishi ya Iran," madai ambayo Tehran iliyakataa hapo awali.
Aliyasema hayo wakati Iran na Marekani zikituma ishara za mseto kuhusu mustakabali wa mazungumzo yao ya nyuklia yaliyoanza tena hivi karibuni. Tehran imekana kutuma mawasiliano yoyote rasmi kwa Washington, huku Pentagon ikijiandaa kwa uwezekano wa kupelekwa kwa manowari ya pili ya kubeba ndege Mashariki ya Kati.
Netanyahu alifika katika Ikulu ya White House Jumatano asubuhi kwa ajili ya mkutano na Rais wa Marekani Donald Trump, ambao ni mkutano wa saba tangu kuanza kwa awamu ya pili ya madaraka ya Trump. Baada ya mkutano wa takriban saa tatu, alisema huenda masharti yamefikiwa kwa ajili ya makubaliano mazuri kati ya Marekani na Iran.
"Mazingira ambayo Trump anayaandaa, pamoja na hali ambayo lazima waelewe kwamba hawakuwa sahihi mara ya mwisho walipokosa kufanya makubaliano, hayo huenda yanaweza kuwa masharti kwa ajili ya kufikia makubaliano mazuri," amesema Netanyahu kabla ya kuondoka Marekani na kurudi Israeli bila kufanya mkutano na waandishi wa habari au kutolewa taarifa.
Licha ya waziri mkuu huyo kusukuma msimamo mkali zaidi, Trump amesisitiza kupendelea kwake matokeo ya mazungumzo muda mfupi baada ya mkutano wao huo wa faragha.
Hali inayofuatiliwa zaidi ni kuwa Iran imechora wazi mstari mwekundu kuhusu uwezo wake wa kurutubisha uraniamu na kukataa kupanua mazungumzo zaidi ya faili la nyuklia.
Mapema siku ya Jumatano, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Nchi la Iran Ali Larijani alikiambia Kituo cha Televisheni cha Al Jazeera cha Qatar katika mahojiano wakati wa ziara yake Doha kwamba mazungumzo hayo kati ya Marekani na Iran yalilenga kabisa mpango wa nyuklia wa Iran, siyo masuala mengine.
Pia amekataa kuwepo kwa urutubishaji wowote wa uraniamu kwenye ardhi ya Iran, akirejelea mahitaji ya Iran ya nishati na dawa, na amekanusha uwezekano wa mazungumzo juu ya uwezo wa makombora au washirika wa kikanda.
Jarida la Wall Street liliripoti Jumatano wiki hii kwamba Pentagon iko tayari kupeleka manowari ya pili ya kubeba ndege katika eneo la Mashariki ya Kati ndani ya wiki mbili, hatua ambayo inamaanisha uwepo wa mara ya kwanza kwa wakati mmoja kwa manowari mbili katika eneo hilo tangu Machi 2025 wakati manowari za USS Harry S. Truman na USS Carl Vinson zote zilipokuwa Mashariki ya Kati kupigana na Wahouthi nchini Yemen.
Picha hii iliyopigwa Februari 9, 2026 ikionyesha mandhari ya Jiji la Tehran, Iran. (Xinhua/Shadati)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



